Meneja
wa kiwanda cha TBL ilala jijini Dar es Salaam, Calvin Martin, akiwa na
wafanyanyakazi wa kiwanda hicho wakikabidhi masada wa vipuri kwa Mkuu wa
Kituo cha Polisi Ilala jijini Dar es Salaam, ASP Nyararo Otuma,kwa
ajili ya kuboresha usafiri wa Jeshi hilo.
Meneja
wa masuala Endelevu wa TBL,Irene Mutiganzi na Mkuu wa Kituo cha Polisi
Ilala jijini Dar es Salaam, ASP Nyararo Otuma, wakisaini nyaraka za
makabidhiano ya vipuri hivyo.
Baadhi ya wafanyakazi wa TBL Ilala, wakishuhudia makabidhiano hayo katika hafla iliyofanyika katika kiwandani.
Mkuu
wa Kituo cha Polisi Ilala jijini Dar es Salaam, ASP Nyararo Otuma,
akiongea na baadhi ya wafanyakazi wa TBL Ilala jijini Dar es
Salaam Wakati wa hafla hiyo
Kampuni
ya TBL chini ya kampuni ya Kimataifa ya ABInBev,imekabidhi masada wa
vipuri vya kukarabati magari ya kituo cha polisi cha Ilala akiwa ni
mwendelezo wake wa kuunga mkono jitihada za Serikali za kukabiliana na
changamoto mbalimbali mojawapo ikiwa ni kuimarisha usalama kupitia
kuboresha usafiri katika Jeshi hilo.
Msaada huo ulikabidhiwa na Meneja wa Kiwanda cha TBL cha Ilala, Calvin
Martin na ulipokelewa naMkuu wa Kituo cha Polisi Ilala jijini Dar es
Salaam, ASP Nyararo Otuma,ambaye alishukuru kampuni hiyo kwa kuona
umuhimu wa kusaidia taasisi za Serikali sambamba na kufanya nazo kazi
kwa kariibu katika kufanikisha kampeni mbalimbali zenye kunufaisha
jamii.
Meneja wa kiwanda cha Ilala,Calvin Martin, alisema kuwa TBL, itaendelea
kuunga mkono jitihada za Serikali za kusaidia kukabiliana na changamoto
mbalimbali kama ambavyo imetoa vipuri (Shock Absorber) kwa ajili ya
kufanikisha kutengeneza magari ya kituo cha Polisi cha Ilala, kwa ajili
ya kuboresha usafiri wa askari wakati wa kutekeleza majukumu yake ya
ulinzi na huduma mbalimbali katika jamii.
Aliongeza kusema kwa muda mrefu kampuni ya TBL imekuwa ikifanya kazi kwa
karibu na Jeshi la Polisi katika kufanikisha kampeni zake mbalimbali za
kijamii hususani zinazohusu usalama barabarani,kupinga vitendo vya
Ukatili wa kijinsia na kampeni ya kuhamasisha matumizi yenye vinywaji
vyenye kilevi kistaarabu.




No comments :
Post a Comment