Kaimu
Kamishna Jenerali wa Magereza, Kamishna wa Magereza, Uwesu
Ngarama(kulia) ambaye pia ni Kaimu Katibu wa Sekretarieti ya Bodi ya
Taifa ya Parole akitoa taarifa fupi kabla ya kumkaribisha rasmi
Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Parole, Mhe. Augustino Mrema(kushoto)
afungue rasmi Kikao cha 41 cha kujadili Wafungwa waliopendekezwa
kunufaika/kutonufaika katika mpango wa Parole. Kikao hicho cha siku moja
kimefanyika leo Julai 12, 2019, katika Bwalo la Maafisa Magereza,
lililopo Ukonga, Jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti
wa Bodi ya Taifa ya Parole, Mhe. Augustino Mrema(hayupo pichani)
akifungua kikao cha 41 cha kujadili Wafungwa waliopendekezwa
kunufaika/kutonufaika katika mpango wa Parole.
Wajumbe
wa Bodi ya Taifa ya Parole wakifuatilia majadiliano ya wafungwa
waliopendekezwa kunufaika/kutonufaika katika mpango wa Parole leo Julai
12, 2019, katika Bwalo la Maafisa Magereza, lililopo Ukonga, Jijini Dar
es Salaam.
Baadhi ya Wajumbe Sekretarieti wakifuatilia kwa makini majadiliano katika kikao hicho.
Mwenyekiti
wa Bodi ya Taifa ya Parole, Mhe. Augustino Mrema(meza kuu) akiongoza
Kikao cha 41 cha Bodi hiyo(Picha zote na Jeshi la Magereza).Na Lucas Mboje, Jeshi la Magereza
BODI
ya Taifa ya Parole ya Awamu ya Tano imeelezea mafanikio mbalimbali
katika kipindi cha miaka mitatu ambapo Bodi hiyo imewezesha kuachiliwa
jumla ya wafungwa 648 katika mpango huo wa Parole na hadi sasa hakuna
mfungwa yeyote aliyevunja masharti ya Parole na kurudishwa gerezani.
Hayo
yamesemwa mapema leo na Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Parole, Mhe.
Agustino Mrema katika Kikao cha 41 cha Bodi hiyo kilichofanyika katika
Ukumbi wa Maafisa Magereza Ukonga, jijini Dare es Salaam.
“Jumla
ya wafungwa 666 wamejadiliwa na Bodi ya Taifa ya Parole katika vikao
vyake saba vilivyofanyika na kupendekeza kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi ambapo wafungwa 648 wamenufaika na mpango huo na wafungwa 18
hawakupendekezwa kutokana na sababu mbalimbali”. Amesema Mhe. Mrema.
Amesema
kuwa katika utendaji wa Bodi yake kwa miaka mitatu umechangia kuimarika
kwa hali ya utulivu na usalama ndani ya magereza kwa wafungwa kwani
wamekuwa na matumaini makubwa ya kuingizwa kwenye mpango huo sanjari na
kupokea programu za urekebishaji katika magereza mbalimbali nchini.
Mafanikio
mengine ni kuwa Wafungwa walioachiliwa katika mpango huo katika kipindi
hiki wameshiriki na wanaendelea kushiriki vyema katika shughuli za
maendeleo katika jamii zao ikiwemo kuziangalia na kuzihudumia familia
zao; hivyo kuipunguzia Serikali gharama za kuwahudumia wafungwa hao kama
wangekuwepo magerezani.
Aidha,
Mhe. Mrema amezungumzia changamoto mbalimbali ambazo zinaikabili Bodi
hiyo ikiwemo ufinyu wa bajeti katika kufanikisha shughuli za Bodi.
Changomoto zingine ni katika maeneo ya kiutawala, kisheria ambazo hata
hivyo amesema hatua mbalimbali za utatuzi zinaendelea kufanyiwa kazi na
mamlaka husika.
“Bodi
hii ya tano imefanikiwa kwa kiasi kikubwa katika kutekeleza majukumu
yake katika kipindi cha miaka mitatu, licha ya changamoto hizo
nilizozitaja, kipekee nitoe shukrani za dhati kwa wajumbe wa Bodi kwa
ushirikiano wao kwangu. Pia natoa shukrani za kipekee kwa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kwa
kuniteua kuwa Mwenyekiti wa Taifa wa Bodi hii katika kutekeleza matakwa
ya Sheria ya Bodi za Parole Sura ya 400”. Amesema Mhe. Mrema.
Bodi
ya Taifa ya Parole ya Awamu ya Tano ilizinduliwa na kuanza kufanya kazi
zake Machi 21, 2019 na inatarajia kumaliza muda wake wa kuwa madarakani
kwa miaka mitatu ifikapo Julai 16, 2019.
No comments :
Post a Comment