Friday, July 12, 2019

RAIS WA UGANDA YOWERI MUSEVENI KUFANYA ZIARA YA SIKU MOJA NCHINI

Rais wa Jamhuri ya Uganda, Mhe. Yoweri Kaguta Museveni kesho Jumamosi tarehe 13 Julai, 2019 atafanya Ziara Binafsi ya siku 1 moja hapa nchini.
Mhe. Rais Museveni atamtembelea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kijijini kwake Mlimani katika Wilaya ya Chato Mkoani Geita.

Akiwa Chato, Mhe. Rais Museveni atafanya mazungumzo na mwenyeji wake Mhe. Rais Magufuli.
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Chato

12 Julai, 2019

No comments :

Post a Comment