Friday, July 12, 2019

MAKAMU MWENYEKITI WA CCM (BARA), PHILIP MANGULA ATEMBEELA BANDA LA BoT NA KUKUTA MAENDELEO MAKUBWA UKILINGANISHWA NA ILIPOANZISHWA 1966

 
 Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanznaia Bara, Bw. Philip Mangula, (kulia) akitazama noti za Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ili kutofautisha zile halisi na feki, huku akipata usaidizi kutoka kwa Meneja Msaidizi (Uhusiano na Itifaki) wa BoT Bi. Vicky Msina, alipotembela banda la BoT kwenye Maonesho ya 43 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam Julai 12, 2019.
 Meneja Msaidizi wa Benki Kuu, (BoT), kutoka Kurugenzi ya Huduma za Kibenki, Bw.Abdul M. Dollah (katikati), akifafanua mambo mbali mbali mbele ya Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Bw. Philip Mangula (kushoto), wakati alipotembelea banda la BoT Julai 12, 2019. Wanaoshuhudia ni Bi. Vicky Msina kulia na (wapili kushoto) ni Afisa wa Tantrade waandaaji wa maonesho hayo.
Bw. Mangula akipatiwa maelezo kuhusu   Chuo Cha Benki Kuu ya Tanzania Mwanza.


 Bw. Mangula akipatiwa maelezo katika Kurugenzi ya Usimamizi wa maduka ya kubadilisha fedha za kigeni
 Bw. Mangula akiwa katika Dawati la Utatuzi wa Malalamiko ya Wateja Huduma za Kibenki.
 Bw. Mangula akipatiwa maelezo kuhusu utengenezaji fedha kutoka kwa Meneja Msaidizi wa Benki Kuu, (BoT), kutoka Kurugenzi ya Huduma za Kibenki, Bw.Abdul M. Dollah (wakwanza kulia).

Bw. Mangula akiwa kwenye meza ya Chuo cha Benki Kuu Mwanza.
 
 NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanznaia Bara, Bw. Philip Mangula ametembelea banda la Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kwenye maonesho yanayoendelea ya biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam kwenye viwanja vya Mwalimu J.K Nyerere leo Julai 12, 2019 na kusema ameshuhudia mabadiliko na maendeleo makubwa ukilinganisha na ilivyokuwa mwak 1966 wakati chombo hicho kilipoanzishwa.
"Tangu tumeanza Benki Kuu mwaka 1966 mpaka sasa mabadiliko mengi na makubwa nimeshuhudia namna watu wanavyoweka noti zinachakaa, lakini unaweza kuzileta huku zikabadilishwa na ukapewa mpya, lakini jinsi wanavyotambua noti feki kwakweli nimepata utaalamu mkubwa, leo nimepata knowledge  (elimu) kubwa Zaidi." Alifafanua Bw. Mangula.
Katika maonesho hayo wananchi wanaotembeela banda la BoT wanapata fursa ya  kupewa elimu ya kazi zinazofanywa na Kurugenzi mbalimbali za BoT zikiwemo Kurugenzi ya Usimamizi Sekta ya Fedha, Kurugenzi ya Huduma za Kibenki, Kurugenzi ya Mifumo ya Malipo ya Taifa, Bodi ya Bima ya Amana, Dawati la Utatuzi wa Malalamiko ya Wateja Huduma za Kibenki, namna fedha zinavyotengenezwa, namna ya kupata chenji za fedha mbalimbali kama vile noti na sarafu.

No comments :

Post a Comment