Friday, July 12, 2019

KAMATI YA MAUDHUI TCRA YAANZA ZIARA YA KIKAZI KUTEMBELEA VYOMBO VYA UTANGAZAJI KANDA YA KASKAZINI

Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha Bw. Richard Kwitega (Katikati) katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Kamati ya Maudhui ya TCRA, pamoja na Kaimu Mkuu wa Kanda ya Kaskazini waliomtembelea ofisini kwake, jijini Arusha leo. Wajumbe hao wako katika ziara ya kuvitembelea vyombo vya utangazaji vya Kanda ya Kaskazini ili kutoa elimu ya uandaaji na usimamiaji wa maudhui bora ya uchaguzi nchini. Maudhui ya Vyombo vya utangazaji ni muhimu katika kuhimiza amani na utulivu wakati wote wa kipindi cha uchaguzi. Tanzania inatazamia kufanya chaguzi za Serikali za Mitaa baadae mwaka huu 2019 na Uchaguzi Mkuu mwakani 20120.

No comments :

Post a Comment