Makamu wa Pili wa Rais, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi (wapili kushoto), akimkabidhi Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Ben Mwaipaja tuzo ya mshindi wa pili miongoni mwa
mabanda bora ya wizara na taasisi za serikali.
Makamu wa Pili wa Rais, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi (wapili kushoto), akimkabidhi Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Ben Mwaipaja tuzo ya mshindi
wa pili katika ubunifu wa mfumo wa ukusanyaji maduhuli ya serikali (Gepg) ambao
umerahisisha mfumo wa malipo kwa wafanyabiashara, wawekezaji na usimamizi wa
maonesho hayo.
Makamu wa Pili wa Rais, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi, akihutubia. |
Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Innocent Bashungwa akihutubia. |
Bw. Mwaipaja akionesha moja ya tuzo hizo.
NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
WIZARA
ya Fedha na Mipango, imetwaa tuzo mbili mtawalia kwenye Maonseho ya 43
ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam yanayofikia kilele Jumamosi
Julai 13, 2019.
Katika hafla ya ufungaji rasmi wa maonesho hayo kwenye ukumbi wa Rashid Mfaume Kawawa (Ceremonial dome) Julai
11, 2019 Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,
Balozi Seif Ali Iddi alikabidhi tuzo hizo moja baada ya nyingine, kwa
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Fedha na Mipango,
Bw. Ben Mwaipaja.
Akizungumzia tuzo hizo Bw, Mwaipaja alisema moja ni ya mshindi
wa pili katika ubunifu wa mfumo wa ukusanyaji maduhuli ya serikali (Gepg) ambao
umerahisisha mfumo wa malipo kwa wafanyabiashara, wawekezaji na usimamizi wa
maonesho hayo huku tuzo nyingine ikiwa ni ya mshindi wa pili miongoni mwa
mabanda bora ya wizara na taasisi za serikali.
Maonesho
hayo yanayofanyika kwenye viwanja vya Mwalimu J.K. Nyerere maarufu
Sabasaba, barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam, yamebeba kauli mbiu
isemayo "Usindikaji wa Mazao ya Kilimo kwa maendeleo endelevu ya viwanda."
No comments :
Post a Comment