Kamishna Mhifadhi wa Misitu Prof. Dos Santos Silayo akikagua baadhi ya maofisa wa Jeshi Usu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania mara baada ya kuwasili makao makuu ya Ofisi za Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania |
Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Tehama, Harold Chipanha akimuongozo Kamishna Mhifadhi wa Misitu Prof. Dos Santos Silayo kwenda kwenye ukumbi wa mikutano wa Ngorongoro uliopo makuu ya Ofisi za Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) kuzungumza na watumishi. |
Kamishna
Mhifadhi wa Misitu Prof. Dos Santos Silayo katika muonekano mpya mara
baada ya kuwasili makao makuu ya Ofisi za Wakala wa Huduma za Misitu
Tanzania akiwa na jukumu la kuwaongoza maofisa wake kwenye muundo wa
kijeshi.
Kamishna
Msaidizi Mwandamizi wa Tehama, Harold Chipanha akimpigia saluti
Kamishna Mhifadhi wa Misitu Prof. Dos Santos Silayo mara baada ya
kuwasili makao makuu ya Ofisi za Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania
jijini Dar es Salaam kwa mara ya kwanza tangu kuvishwa cheo hiko cha
kijeshi Julai 9,2019 wilayani Chato mkoani Geita.
picha ya pamoja na na maofisa waJeshi Usu
Maafisa
wa Jeshi Usu wa TFS wakifurahia jambo wakati Kamishna Mhifadhi wa
Misitu Prof. Dos Santos Silayo alipokuwa akizungumza nao kw amara ya
kwanza tangu aanze kutekeleza majukumu yake akiwa si raia tena.
Na Tulizo Kilaga,TFS
KWA
mara ya kwanza tangu avishwe cheo cha Kamishna Mhifadhi wa Misitu na
Dkt Hamisi Kigwangalla, Waziri wa Maliasili na Utalii na hatimaye kula
Kiapo cha Utii na uadilifu mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Magufuli Julai 9, 2019, Kamishna
Prof. Dos Santos Silayo amewasili makao Makuu ya Wakala wa Huduma za
Misitu Tanzania (TFS), Jengo la Mpingo jijini Dar es salaam na
kupokelewa na Viongozi Waandamizi na watumishi wa TFS.
Akizungumza
na watumishi wake mara baada ya kuwasili ofisini hapo, Kamishna Prof.
Silayo alisema mabadiliko yanayotokea katika sekta ya maliasili
yamepelekea pia kubadili mfumo wa usimamizi na utendaji wetu toka ule wa
Kiraia kwenda Jeshi Usu.
“Namshukuru
Mungu kuwa sehemu ya mabadiliko hayo. Hatua hiyo ikapelekea kuvishwa
cheo cha Kamishna Mhifadhi wa Misitu na Mhe Dkt. Hamisi Kigwangalla,
Waziri wa Maliasili na Utalii na kula Kiapo cha Utii mbele ya Mheshimiwa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi
ya Ulinzi na Usalama Dkt. John Pombe Magufuli siku ya tarehe 9 Julai
2019.
“Mabadiliko
haya yanalenga kujenga uwezo wa taasisi, uwezo wa watumishi ikiwa ni
pamoja na kuwajengea ari, uzalendo, weledi na ujasiri katika kusimamia
rasilimali za misitu na nyuki,” alisema Kamishna Prof. Silayo.
Kamishna
Prof. Silayo anasema uwezo wa watumishi wa TFS utaenda sambamba na
weledi katika matumizi ya mbinu na vifaa vya kisasa vinavyoweza kumudu
mabadiliko ya changamoto za uhifadhi kuanzia usalama wao pamoja na
usalama wa mali zenyewe unaotokana na kuongezeka kwa mbinu za kihalifu
kila wakati.
Aidha
Prof. Silayo alitoa shukurani kwa Mheshimiwa Rais na viongozi wote wa
wizara ya Maliasili na Utalii kwa hatua hiyo waliyofikia ambayo anaamini
itasaidia kukuwa kwa sekta ya misitu nchini na kuongeza ushirikiano na
wadau wengine hususani wananchi katika kusimamia misitu yetu.
Akiongea
kwa njia ya simu Naibu Kamishna wa Huduma Saidizi, Emmanuel Wilfred
alisema mabadiliko hayo yamepelekea kubadili mfumo wa usimamizi na
utendaji wa TFS toka ule wa Kiraia kwenda Jeshi Usu na hivyo kulazimu
watumishi wote kwenda kwenye mafunzo.
“Tunaendelea
kutoa mafunzo kwa watumishi wachache waliobaki na kwa wale
waliokwishakwenda kwenye mafunzo tunakamilisha taratibu ili Kamishna
aweze kuwatunuku vyeo vyao, lakini niwatake wafanyakazi wote kuenda
sambamba na mabadiliko kwa kasi hitajika,” alisema Kamishna Msaidizi
huyo.
Rosemary
Sabida mmoja wa watumishi wa TFS anasema mabadiliko hayo yataisaidia
TFS kukabiliana na changamoto mbalimbali za uhifadhi nchini.
Jumla
ya Makamishna wanne, Kamishna wa Uhifadhi wa Shirika la Hifadhi za
Taifa (TANAPA) Dkt Allan Kijazi, Kamishna wa Uhifadhi wa Misitu toka
Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Prof Dos Santos Silayo na
Kamishna wa Uhifadhi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania
(TAWA) Dkt.James V. Wakibara pamoja Kamishna wa Uhifadhi wa Mamlaka ya
Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA), Freddy Manongi walivishwa vyeo vya
kijeshi Julai 9, 2019 katika sherehe za Uzinduzi wa Hifadhi ya Taifa ya
Burigi – Chato zilizofanyika wilayani Chato mkoani Geita.
No comments :
Post a Comment