Mkuu
wa mkoa wa Katavi Juma Homera ameapa kupambana na wanaotorosha dhahabu
huku mpaka sasa watu wawili wakishikiliwa na jeshi la polisi kwa
kununua dhahabu kinyume cha sheria mkoani humo.
RC
Homera akiwa ziarani katika migodi mbalimbali ikiwemo Dilifu ambao ni
mgodi wa wachimbaji wadogo na mgodi mkubwa wa Katavi na Kapufi mining
alieleza anachotaka wachimbaji wadogo wakauuze madini yao katika soko la
madini la mkoa huo.
Homera
alianza majukumu ya ukuu wa mkoa ikiwa soko limeshafanya biashara kwa
kununua dhahabu gram 238, May 23/2019 jambo ambalo lilimfanya aanze
kufatilia na kubaini dhahabu nyingi inayopatikana Mkoani Katavi inauzwa
nje ya mkoa wa Katavi nakupelekea soko hilo kusua sua.
Kufuatia
jambo hilo limemfanya Homera kuyafanyia kazi mapungufu ya soko hilo,
mpaka sasa ununuzi na uuzaji wa madini ni Grams 6317.2 sawa na Kg 6 na
Grams 317.2 yenye thamani ya Tshs.Million 519,155,127.56 zimenunuliwa
kwa kipindi cha Mei na June 30/2019 na serikali kupata mrahaba
(Royality7%) Tsh Milioni 36,340,858.92 na Service levy 0.3% Tsh.milioni
1,401,718.85.
Aidha
ameimarisha mifumo ya Benk mbili katika soko hilo na ameendelea kuwa
bana mablokers na wanunuzi wenye leseni na wachimbaji mbalimbali
kuhakikisha pia wanauza madini yao kwenye soko la mkoa ili tujenge
uchumi wa Tanzania na kumuunga mkono Rais wetu Dkt.John Joseph Pombe
Magufuli katika kuinua uchumi na miundombinu ya nchi hii kwa kulipa kodi
No comments :
Post a Comment