Monday, July 1, 2019

ESRF YAANDAA WARSHA KUBORESHA MRADI WA PSDS 2006


Mkuu wa Idara ya Utafiti na Machapisho wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Kijamii (ESRF), Profesa Fortunata Makene akitoa neno la ukaribisho kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa ESRF, Dk. Tausi Kida wakati wa warsha ya kitaifa ya utekelezaji wa mkakati wa maendeleo kwa nchi za Afrika Mashariki unaozingatia mchango wa sekta binafsi (EAC- PSDS) iliyoandaliwa na ESRF mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam. (EAC- PSDS) iliyoandaliwa na ESRF mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
Ofisa wa kitengo cha maendeleo ya sekta binafsi Ofisi ya Waziri Mkuu, Diana Makule akiwasilisha mada ya mtazamo wa jumla wa PSDS 2006 na matokeo ya utekelezaji wake wakati wa warsha iliyoandaliwa na ESRF mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
Mtaalamu wa masuala ya tabia nchi kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais, Martha Ngalowera akiwasilisha mada kuhusu uchakataji wa mazao ya kilimo katika mradi wa PSDS 2006 kwa kuangalia vifungu vinavyohusiana na tabia nchi kwenye warsha iliyoandaliwa na ESRF mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa warsha, Meneja Ufuatiliaji na Tathmini , Kituo cha Taasisi ya Maendeleo Endelevu (CSDI), Dk Isaack Nguliki akizungumzia biashara kuchagiza uchakataji wa mazao ya kilimo kwa kuangalia vifungu vinavyohusiana na tabia nchi katika PSDS kwenye warsha iliyoandaliwa na ESRF mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
Bi. Rehema Mbugu kutoka Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF)akiongoza majadiliano ya mtazamo wa jumla wa PSDS 2006 na matokeo ya utekelezaji wake wakati wa warsha iliyoandaliwa na ESRF mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
Washiriki wakishiriki majadiliano wakati wa warsha ya kitaifa ya utekelezaji wa mkakati wa maendeleo kwa nchi za Afrika Mashariki unaozingatia mchango wa sekta binafsi (EAC- PSDS) iliyoandaliwa na ESRF mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
Mshehereshaji ambaye pia ni Mkuu wa kitengo cha Uwezeshaji na Utawala Bora wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Danford Sango akisisitiza jambo wakati wa warsha ya kitaifa ya utekelezaji wa mkakati wa maendeleo kwa nchi za Afrika Mashariki unaozingatia mchango wa sekta binafsi (EAC- PSDS) iliyoandaliwa na ESRF mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Idara ya Utafiti na Machapisho wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Kijamii (ESRF), Profesa Fortunata Makene akifafanua jambo wakati wa warsha ya kitaifa ya utekelezaji wa mkakati wa maendeleo kwa nchi za Afrika Mashariki unaozingatia mchango wa sekta binafsi (EAC- PSDS) iliyoandaliwa na ESRF mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
**
Wakati Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) imejikita katika kutaka kuendeleza mkakati wa sekta binafsi (PSDS) 2018-2022, wenye lengo la kuweka mazingira mazuri ya biashara yatakayochochea ushindani ndani ya sekta binafsi kwa kuongeza uwekezaji, tija na biashara, Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF) imekutanisha wadau kuangalia namna ya kuboresha mkakati huo.
Katika warsha hiyo wadau walizungumzia na kuainisha mambo mbalimbali yenye lengo la kuuwezesha Mkakati huo kutoa mchango wenye uelewa wa mabadiliko ya tabia nchi, uzalishaji wenye msukumo wa kibiashara na uchakataji wa bidhaa za kilimo.
Dk. Tausi Kida Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), akifungua warsha hiyo mwishoni mwa wiki alitaka washiriki kuwa makini ili kuweza kuona namna gani wanaweza kuimarisha mkakati huo.
Akishawishi umakini katika warsha hiyo ya kitaifa ya utekelezaji wa mkakati wa maendeleo kwa nchi za Afrika Mashariki unaozingatia mchango wa sekta binafsi (EAC- PSDS), alisema bila umakini mchango wa mkakati huo hautaonekana.
Katika warsha hiyo wadau walizungumzia upenyo wa maendeleo endelevu katika uchakataji wa bidhaa za kilimo.
Warsha hiyo ikiwa ni sehemu ya awamu ya pili ya mradi wa kuendeleza kilimo katika nchi za Afrika mashariki unaoangalia mabadiliko ya tabia nchi na mahusiano ya kibiashara katika nchi hizo- (PACT EAC2). Mradi huo umekuwa ukiendeshwa na ESRF kwa kushirikiana na CUTS International yenye makao makuu yake mjini Geneva Uswisi.
Mkurugenzi huyo wa ESRF alisema kwamba toka mwaka 2015 mradi umekuwa ukifanya majadiliano ya kina kwa sekta mbalimbali ambazo nyingi ni mtambuka ili wadau wengi wawe wanajua kwa pamoja mabadiliko ya tabia nchi, mahusiano yao na uzalishaji, biashara, usalama wa chakula na viwanda vya kuchakata bidhaa za kilimo.
Kwa mujibu wa Dk Tausi warsha hiyo ilikuwa na lengo la kuwapa nafasi wadau wote kuangalia njia bora zaidi ya kuwezesha uchakataji endelevu wa viwanda vya bidhaa za kilimo ili kuvipa thamani kupitia sekta binafsi.
Mkurugenzi huyo aliwataka washiriki kujadili kwa kina mchango wa sekta binafsi katika kuchagiza uelewa wa mabadiliko ya tabia nchi, na uendelezaji wa kilimo biashara na usalama wa chakula katika ukanda huu wa Afrika Mashariki.
“Kutokana na ukweli huo napenda mazungumzo yetu ya leo yajikite zaidi katika kufanikisha mkakati wa sekta binafsi kuhusu maendeleo (PSDS) 2018-2022 kuhusu wajibu wake kuendeleza uchakataji wa bidhaa za kilimo endelevu utakaozingatia mabadiliko ya tabia nchi biashara na usalama wa chakula.” alisema Dk Tausi.
Katika warsha hiyo ambapo mada mbili ziliwasilishwa moja ikizingatia mabadiliko ya siasa na sheria nchini na mazingira ya sasa kuhusiana na mkakati huo wa kuwezesha ukuaji wa sekta binafsi na dhana ya uendelezaji wa kilimo biashara katika uhusiano na mabadiliko ya tabia nchi na nyingine.
Mada hizo zimetolewa na wataalamu kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais na Ofisi ya Waziri Mkuu,wakiangalia PSDS ilivyowezeshwa kusaidia sekta binafsi kuchochea uelewa wa mabadiliko ya tabia nchi, kilimo biashara na uchakataji wa bidhaa za kilimo na usalama wa chakula.
Mada hizo ziliwasilishwa na Diana Makule wa Ofisi ya Waziri Mkuu na Martha Ngalowera wa Ofisi ya Makamu wa Rais.

No comments :

Post a Comment