Mwanasheria
Mkuu wa chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania cha Chadema, Tundu
Lissu amesema amehitimisha matumizi ya dawa alizoanza kuzitumia tangu
Septemba 7 mwaka 2017.
Lissu
alianza kutumia dawa hizo Septemba 7 mwaka 2017 baada ya kushambuliwa
kwa risasi zaidi ya 30 akiwa katika makazi yake Area D jijini Dodoma
ambapo tangu wakati huo amekuwa akipatiwa matibabu nje ya nchi.
Katika salamu kwa marafiki zake alizozitoa leo Jumatano Julai 31, 2019, kupitia ukurasa wake wa Instagram, Lissu ameandika;
Hello Marafiki wa Mimi,
Habari
za masiku mengi. Sijawasemesha kwa kitambo kidogo. Nisameheni bure,
nafikiri mnafahamu jinsi ambavyo mambo yamekuwa mengi. Nina mambo
mawili, nayo ni mema tu. .
La
kwanza linahusu hali yangu ya afya. Leo tarehe 31 Julai, 2019, ni siku
ya kwanza tangu niliposhambuliwa Septemba 7, 2017, situmii dawa ya aina
yoyote..
Kwa
maelekezo ya madaktari wangu, jana ilikuwa siku ya mwisho ya mimi
kutumia madawa ambayo nimeyatumia tangu siku niliposhambuliwa..
Na
jana hiyo hiyo nilitimiza mwezi mzima tangu niache kutumia magongo.
Ijapokuwa bado nachechemea kwa sababu ya goti kutokukunja sawa sawa,
sasa ninatembea bila msaada wa magongo. .
Safari
yangu, na yetu, ndefu ya matibabu itakamilika Agosti 20 nitakapokutana
na timu ya madaktari wangu kwa ajili ya vipimo vya mwisho na ushauri. .
Baada ya hapo itakuwa ni maandalizi ya kurudi makwetu. Hakutakuwa na sababu tena ya kitabibu ya mimi kuendelea kukaa Ulaya. .
Kwa
vile tumekuwa pamoja kwenye safari hii ndefu, hatuna budi kupongezana
na kumshukuru Mungu kwa hatua hii nzuri nilikofikia. Mimi na familia
yangu hatutachoka kuwashukuru sana kwa kuwa pamoja nasi katika kipindi
chote hiki kigumu. Mungu awabariki sana. .
La
pili linahusu ubunge wangu. Tangu Spika Ndugai anivue ubunge, sijasema
maneno mengi sana, zaidi ya kusema kwamba tutaenda Mahakama Kuu kupinga
uamuzi huo. .
Kesi
za ubunge, kama zilivyo kesi zote za uchaguzi wa kisiasa, ni kesi za
kisiasa. Ni mwendelezo wa mapambano ya kisiasa katika uwanja tofauti. .
Kwa
sababu hiyo, ni kesi nyeti na za kipekee sana. Zinahitaji umakini
mkubwa katika kuziandaa na kuziendesha. Nina uzoefu mkubwa nazo, kwa
sababu nimezifanya sana tangu 2005.
Sasa
ninaweza kuwafahamisha kwamba mimi na timu ya mawakili wangu tuko
tayari kuingia Mahakama Kuu ya Tanzania. Tutafanya hivyo muda wowote
kuanzia leo. Maandalizi yote yanayohitajika yamekamilika.
Tunataka
kuiomba Mahakama Kuu itoe jibu la swali alilouliza Spika Ndugai na
walio nyuma yake: je, Spika wa Bunge la Tanzania ana uwezo kikatiba na
kisheria, wa kufuta ubunge wa mbunge yeyote yule, kwa sababu yoyote ile,
bila kumuuliza mbunge husika jambo lolote kuhusu sababu za kumfuta
ubunge huo??? .
Nitawajulisheni
mara moja kesi hii itakaposajiliwa rasmi. Kama itawapendeza, nitawaomba
mtakaopata nafasi kuhudhuria mahakamani, kwa niaba yangu, wakati wote
kesi hiyo itakapokuwa inaendelea. .
Nilitaka kuwashirikisheni haya kwa leo. Nawashukuruni sana na Mungu awabariki sana.
No comments :
Post a Comment