Kamanda
wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa, ametolea
ufafanuzi kifo cha mtumishi wa Wizara ya fedha, Leopard Lwajabe (56),
ambaye mwili wake ulipatikana ukiwa umening’inia kwenye mti wa muembe
katika kijiji cha Mgoza wilayani Mkuranga.
Mambosasa
amesema uchunguzi wa awali ulibaini kuwa eneo la tukio hakukuwa na
viashiria vyovyote vya kujitetea wakati wa tukio na kwamba mwili wa
marehemu hakukuwa na jeraha lolote isipokuwa shingoni kulikokuwa
kumefungwa kamba iliyotumika kujingonga.
Ametoa
ufafanuzi huo leo Jumatano Julai 31, alipokuwa akizungumza na waandishi
wa habari ambapo amesema mnamo Julai 26 mwaka huu Polisi Kanda Maalum
ya Rufiji walipokea taarifa kutoka kwa Mwenyekiti wa kijiji cha Mgoza,
Mohamed Said (68), kwamba kumeonekana mwili wa mwanaume ukiwa unang’inia
kwenye mti wa muembe na polisi walipofika waliukuta mwili huo ukionesha
mhusika amenyinyonga.
“Julai
29, mwaka huu walipatikana ndugu wawili wa marehemu ambao ni Chumila
Mwalimu mkazi wa Manyara na Jonathan Herman ambaye ni mfanyakazi
mwenzake na marehemu ambao walifanikiwa kuutambua mwili na kueleza kuwa
marehemu alitoka nyumbani kwake kwenda ofisini akiwa na dereva wake na
baadae alimtuma dereva akamchukulie simu nyumbani kwake Kinyerezi na
baada ya hapo marehemu alitoweka ofisini na kwenda kusikojulikana hadi
alipogundulika amejinyonga,” amesema.
“Mnamo
Julai 29, wafanyakazi waligundua kuwa marehemu aliacha notebook mezani
kwake iliyokuwa na mgawanyo wa mali zake ambapo aliruhusu kati ya
ng’ombe anaofuga wanne watumike katika msiba wake na pia simu aliyomtuma
dereva iligundulika kuwa imeshafutwa kumbukumbu zote,” amesema.
Aidha
amesema mwili wa marehemu ulihamishiwa hospitali ya Taifa Muhimbili kwa
uchunguzi zaidi na ilibainika kifo hake kilisababishwa kwa kujinyonga
ambapo chanzo hakijafahamika mpaka sasa na upelelezi uaendelea.
“Mtu
aliyeuawa mahali halafu akaeda kufungwa kuna vitu vinavyokosekana kwa
mfano mtu anayejinyonga lazima aachie haja ndogo na kubwa kwababu ya
nguvu ya roho kutoka na hivyo vyote vimekutwa aneo la tukio,” amesema
Mambosasa.
No comments :
Post a Comment