Na.Amiri Kilagalila-Njombe
Kampuni
ya ujenzi wa barabara ya kichina China Henan international cooperation
group co ltd (CHICO) inayotekeleza mradi wa barabara wa km 53.9
Njombe-Moronga kuelekea wilayani Makete mkoani Njombe.
Imeanza
utekelezaji wa ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa pamoja na bwalo
moja la chakula katika shule ya msingi ramadhani mjini Njombe kutokana
na ombi la Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania aliloomba wakati wa
ziara yake april 10 mkoani hapo mara baada ya Rais Magufuli kuombwa na
wanafunzi wa shule hiyo wakati akiweka jiwe la msingi ujenzi wa barabara
ya Njombe-Makete.
Waziri
wa ujenzi Elias kwandikwa amefika na kukagua shughuli zinazoendelea
katika ujenzi huo na kumshukuru mkandarasi kwa utekelezaji huo.
“Kwanza
nimshukuru sana mheshimiwa Rais alivyoweza kulisukuma jambo hili na
hatimaye tumepata huu mradi lakini pia na hawa wenzetu wa Chico kwa
haraka wameanza utekelezaji kwa kweli mimi ninashukuru sana”alisema
Kwandikwa
Lusekelo
kijalo ni injinia wa kampuni hiyo amesema ujenzi wa majengo hayo
unategemewa kukamilika kabla ya mwezi mmoja na nusu kuisha huku ujenzi
huo ukigharimu karibu milioni 240 pindi utakapokamilika
Mwalimu
mkuu wa shule hiyo Ephrahim sanga amesema mradi huo ni mkubwa katika
shule hiyo kwa kuwa ina wanafunzi 1552 na kupelekea kuwa na uhaba wa
vyumba vya madarasa.
“Mimi
hapa nina wanafunzi 1552 wavulana 648 na wasichana 604 vyumba vyetu vya
madarasa ni vichache sana havitoshelezi,ingawa tulikuwa na mpango wa
kujenga shule nyingine mpya lakini mh.Rais ametutangulia kwa kweli
tunashukuru tukaona tuanzie hapa ili tuweze kuigawa shule pawe na
mikondo miwili”amesema mwl.Sanga
No comments :
Post a Comment