
Aliyekuwa
mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu ameeleza sababu ya
kutomwandika barua spika wa Bunge, Job Ndugai kumjuliusha kuwa yupo nje
ya nchi kwa ajili ya matibabu.
Wiki
iliyopita Spika Ndugai alitangaza kumvua ubunge Lissu kwa kile
alichoeleza kuwa kiongozi huyo hajulikana halipo zaidi ya kuonekana nchi
za Ulaya na Marekani.
"Ni
kweli sijawahi kumuandikia Spika Ndugai barua yoyote kuhusu mahali
nilipo, na hali yangu ya kiafya. Sikumwandikia, sio kwa sababu nilisahau
au nilipuuza, bali ni kwa sababu Spika Ndugai alikuwa anafahamu fika
mahali nilipo, na sababu za mimi kuwa huko," amesema Tundu Lissu.
Ameendelea
kwa kusema, "Kwa sheria na taratibu za Bunge, Spika na watendaji wake
wanawajibika kufuatilia hali ya mbunge anayetibiwa nje ya nchi, na kutoa
taarifa za maendeo yake. Sio wajibu wa mbunge mgonjwa kulitaarifu Bunge
juu ya afya yake. Ndugai alipaswa kujua nilipo, na maendeleo yangu."
Lissu,".
Aidha,
Tundu Lissu amesema licha ya Spika wa Bunge, Job Ndugai kudai hakujaza
fomu za mali na madeni za viongozi wa Umma bado ana sifa za kugombea
nafasi yoyote ya uongozi.
"Ili upoteze sifa ya kugombea ubunge au urais sharti uwe na hatia, sasa
mimi sijakutwa na hatia na mahakama au mahakama ya Sekretarieti ya
maadili, Ndugai peke yake hawezi kunitia hatiani bila kunisikiliza."
"Kwa hiyo mimi naweza kugombea nafasi yoyote ya uongozi iwe ubunge au
urais. Kama wanataka nisigombee wanipeleke mahakamani au kwenye mahakama
ya sekretarieti na wakiniuliza kwa nini sijajaza fomu nitawaambia
nitawezaje kujaza nikiwa nje ya nchi," amesema Lissu
Amesema fomu hizo zinapaswa kujazwa na kuziwasilisha kwa njia ya mkono
lakini zinapaswa kusainiwa na wakili wa Tanzania, "Sasa mimi niko
hospitalini Ubelgiji, nawezaje kuzijaza, huku nampata wapi wakili,
nawezaje kuzipeleka kwa mkono? Kwa hiyo walipaswa kuniuliza kwa nini
sijajaza na si kuzungumza sijajaza bila kuwa na sababu."
No comments :
Post a Comment