
Kampuni
ya Safaricom imemteua ofisa mtendaji mkuu wake wa zamani, Michael
Joseph kukaimu nafasi ya mtendaji mkuu iliyoachwa na Bob Collymore
aliyefariki dunia jana Julai 1, 2019.
“Joseph
atashikilia wadhifa huo hadi pale kampuni itakapotoa tangazo jingine
kuhusu uteuzi wa kudumu,” Safaricom ilisema kwenye taarifa yake.
Joseph ni mjumbe katika bodi ya Safaricom na ni mwenyekiti wa sasa wa Shirika la ndege la Kenya, Kenya Airways.
Mwili
wa Collymore aliyechukua wadhifa huo kutoka kwa Joseph Novemba 2010,
utazikwa leo jijini Nairobi katika tukio litakalohusisha tu wanafamilia.
No comments :
Post a Comment