
Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu
amewataka waganga wakuu wa mikoa kuchukua hatua za makusudi kuzuia mbu
waambukizao homa ya dengue na kusisitiza mikoa iliyo mpakani kuchukua
tahadhari ya ugonjwa wa ebola.
Waziri Mwalimu ameagiza hayo jana jijini Dodoma wakati akifungua mkutano
kikao kazi cha viongozi mbalimbali wa hospitali za rufaa za mikoa.
Alisema waganga wakuu ambao maeneo yao yamekumbwa na ugonjwa wa homa ya
dengue na hata mikoa ambayo haijakumbwa na tatizo hilo kuhakikisha
wanaangamiza mazalia kwa kutumia dawa ya viuadudu.
“Ninachotaka
kusisitiza kwa waganga wakuu, najua wenzetu katika wilaya na
halmashauri wanaweza wasituelewe, lakini lazima tuchukue hatua za
kudhibiti mbu, hakuna maajabu mengine ambayo tutayafanya zaidi ya
kudhibiti mbu.
“Kwa
hiyo zile lita chache tunazowapa za dawa kuna wengine wanaona muda
unaenda wanaenda katika mito wanazimwaga, hapana, lazima tukafanye kazi
ya kunyunyuzia katika mazalia ya mbu,” alisema Ummy.
Alisema
mashine hizo zitasambazwa katika baadhi ya mikoa ambayo ina mazalia na
kuwataka waganga wakuu kuwabana wakurugenzi watenge bajeti kwa dawa
hizo.
“Kipekee
nimpokeze Mganga Mkuu wa Dar es Salaam amepambana sana na bahati nzuri
Katibu Tawala wake amemshika vizuri, nasema kwamba ukipewa majukumu
lazima ufanye kazi.
“Tanga
sijaona jitihada zozote kukabiliana na dengue, nasema kweli kwa sababu
mimi natoka Tanga ila watu wanaumwa, Pwani angalau kidogo,” alisema.
Kuhusu
ugonjwa wa ebola, alisema Serikali inaendelea kuchukua hatua za
kukabiliana nao kama utatokea huku akiupongeza Mkoa wa Mwanza kwa jinsi
ulivyojiandaa kuukabili.
“Ebola
bado ni tishio nchini, nilitoa taarifa kwa umma, lakini hakuna ‘case’
mpya zaidi ya zile zilizotokea. Habari mbaya ni kwamba WHO wamesitisha
huduma DRC kwa sababu gari la watumishi limechomwa moto kule.
“Ina
maana itazidi, kwa hiyo tuendelee kuchukua hatua Mwanza, Kigoma, Rukwa
Songwe na Dar es Salaam, ila kipekee nimpongeze Mganga Mkuu wa Mwanza
amefanya kazi nzuri kama mgonjwa atatokea jinsi ya kumhudumia,” alisema.
Ummy
alisema wameagiza mashine 70 za X-ray ambazo zitafungwa katika
hospitali za rufaa za mikoa pamoja na mnashine 20 za X-ray za meno
ambazo nazo zitafungwa katika hospital hizo
No comments :
Post a Comment