
Waziri
wa Mambo ya Nchi za Kigeni wa Iran Mohammed Javad Zarif amesema kuwa
Iran imezidisha ukomo wa viwango vya madini yake ya urani katika
hifadhi zake, uliowekwa chini ya mkataba wa 2015 wa nyuklia.
Shirika la habari la Iran - ISNA limeripoti kuwa Iran ilipitisha kiwango cha ukomo wa kilo 300 kwenye mpango wake.
Marekani
ilijiondoa kwenye mpango huo wa nyuklia mwaka jana na ikaiwekea Iran
vikwazo vikali kama sehemu ya kampeni ya kuiongezea mbinyo mkali.
Kwa
kulipiza kisasi, mnamo Mei 8, Iran ikatangaza kuwa haitaheshimu tena
viwango vya mwisho vilivyowekwa vya hifadhi zake za madini ya urani
yaliyorutubishwa.
Ilitishia
pia kwenda mbali zaidi na kuachana na ahadi zake za nyuklia kama
washirika waliobaki katika mkataba huo, ambao ni pamoja na Uingereza,
China, Ufaransa, Ujerumani na Urusi, hawataisaidia nchi hiyo kutokana na
vikwazo ilivyowekewa na hasa vya kuuza mafuta yake.
Muda
mfupi baada ya tangazo hilo la Iran kutolewa, Shirika la Umoja wa
Mataifa la Kudhibiti matumizi ya nishati ya nyuklia - IAEA
limethibitisha kuwa Iran ilipindukia ukomo wa viwango vyake vya madini
ya urani.
No comments :
Post a Comment