SHIRIKA
la Umeme Nchini (TANESCO) limepewa tuzo ya banda lenye kutoa huduma
bora katika sekta ya Nishati na Madini kwenye maonesho ya 43 ya biashara
ya Kimataifa ya Dar es Salaam yanayofikia kilele Jumamosi Julai 13,
2019.
Makamu
wapili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhe. Balozi Seif Ali
Iddi, ndiye aliyekabidhi tuzo hiyo kwa mwakilishi w aShirika hilo,
wakati wa ufungaji rasmi wa maonesho hayo kwenye ukumbi wa Rashid Mfaume
Kawawa (Ceremonial dome), ulio kwenye viwanja hivyo Julai 11, 2019.
Katika
banda la TANESCO wateja na wanachi waliotembeela banda hilo waliweza
kupata huduma mbalimbali kama zile zinazotolewa kila siku kwenye ofisi
za Shirika hilo.
Kama
vile kujaza fomu za maombi ya mwanzo ya kuombea kuunganishiwa umeme,
kujonea hatua mbalimbali za kuzalisha umeme, lakini pia kununua umeme.
No comments :
Post a Comment