Mkuu
wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda leo Julai 11 ametangaza
Shindano litakakalohusisha Watu wote wanaoendesha Platform za Social
Media ikiwemo Waandishi wa habari Blog, Website, Online Tv, Instagram,
Twitter, Facebook na nyinginezo ambapo watakuwa na jukumu la kuuliza
wananchi maswali kuhusu Jumuiya ya Nchi za SADC ambapo washindi wa
shindano hilo watajishindia kitita cha mamilioni ya Fedha.
RC
Makonda amesema utaratibu wa kushiriki Shindano hilo ni Wahusika kwende
kwenye sehemu za Bar,Saloon,Vijiwe vya bodaboda na Sokoni kisha
kuwahoji wananchi waeleze namna wanavyoifahamu jumuiya ya SADC na
kurusha mahojiano hayo kwenye platform zao ambapo pia wananchi
watakaoweza kutoa majibu kwa ufasaha nao watapatiwa kiasi cha shilingi
Laki moja.
Aidha
RC Makonda amesema Mshindi wa kwanza wa shindano hilo atapatiwa kiasi
cha Shilingi Milioni 3, Mshindi wa pili Milioni 2 na Mshindi wa tatu
Milioni 1 ambapo hafla ya kukabidhi zawadi hizo itafanyika August 05
mwaka huu.
Hata
hivyo RC Makonda amewataka Wamiliki wa Platform za Social Network
kudhihirishia jamii kuwa mitandao yao ina uwezo mkubwa wa kubadilisha
jamii kama ikitumika vizuri ambapo kwa kufanya hivyo watazidi
kuheshimika na pia kuingiza pesa kupitia matangazo.
No comments :
Post a Comment