
Kamanda
wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar Es Salaam (SACP) Lazaro Mambosasa,
amewataka watu wenye taarifa zitakazosaidia upatikanaji wa Raphael
Ongangi, waziwasilishe ofisini kwake ili zifanyiwe kazi.
Akizungumzia
juu ya kauli zilizotolewa na kiongozi wa ACT Wazalendo, Zitto Kabwe
juu ya alipo Raphael, kamanda amesema taarifa hizo ni za mitandaoni,
na kwamba wao hawafanyii kazi mambo ya mitandao.
“Hizo
habari za mitandao kila mmoja anatoa anavyofikiria, cha msingi ambacho
sisi tungeweza kukiona cha maana kama kuna jambo lolote lipelekwe kituo
cha polisi, ofisi yangu ipo, kama kuna mtu ana taarifa alete". alisema
Mambosasa.
Siku
ya Julai Mosi, Mbunge wa Kigoma Mjini na Kiongozi wa Chama cha ACT
Wazalendo, Zitto Kabwe, aliahidi kuwasilisha ushahidi wa eneo alilowekwa
Raphael, kuanzia siku ya kwanza alipotekwa hadi siku ya Jumamosi.
Raia
huyo wa Kenya ambaye ana mke na watoto wawili, alitekwa Juni 24 maeneo
ya Oyserbay Dar es salaam ambapo hadi sasa bado hajapatikana.
No comments :
Post a Comment