
WMU - Dodoma.
Dkt.
Kigwangalla ameyasema hayo jijini Dodoma wakati akizindua rasmi Bodi
hiyo iliyongezewa muda wa miaka 3 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli Aprili 23 mwaka huu.
Akizungumza
wakati wa uzinduzi wa Bodi hiyo amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuiongezea kipindi kingine cha
miaka 3 na kuitaka bodi hiyo iendelee kubuni na kuongeza mbinu mpya za
kutangaza utalii zitakazoleta tija na matokeo ya haraka.
Amewataka
wajumbe wa Bodi hiyo kufanya kazi pamoja na kushirikiana na taasisi
nyingine za Wizara ili kuongezea idadi ya watalii wanaoitembelea
Tanzania akiweka msisitizo katika matumizi ya mifumo ya kisasa ya
mawasiliano ili kupanua wigo wa kutangaza vivutio vya utalii kuliko
ilivyo sasa.
“Bodi
ya utalii mnapaswa kuona fursa zilizopo na kutimiza majukumu mliyopewa
kwa tija na ufanisi zaidi, namna pekee ya kufikia malengo hayo ni lazima
mtumie teknolojia na mbinu rahisi za mawasiliano zenye gharama nafuu
kutimiza majukumu yaleyale ya kutangaza vivutio vya utalii kisasa zaidi”
Amesisitiza.
Ameipongeza
bodi hiyo kwa kazi nzuri inayofanya ya kuendelea kuhamasisha shughuli
za Utalii nchini na kuongeza kuwa kati ya vitu vilivyo iletea heshima
sekta ya utalii Tanzania ni uwepo wa Kaulimbiu ya “TANZANIA
UNFORGETTABLE” ambayo imekua chachu kwa taifa hasa katika kuitangaza
sekta hiyo kitaifa na kimataifa.
Amesema
kupitia kaulimbiu hiyo watalii wengi wanaoitembelea Tanzania
wataendelea kukumbuka mambo mazuri na vivutio vizuri walivyoviona na
kuendelea kuichagua Tanzania kuwa mahali pao pa kufanyia utalii.
Aidha,
ametoa wito kwa Bodi hiyo kuendelea kuweka mazingira na kuongeza soko
la bidhaa za utalii za Tanzania nje ya nchi kupitia maonesho ya
kimataifa na kuwa na mkakati wa kulenga soko husika pamoja na kuonana na
watu watakaouziwa bidhaa moja kwa lengo la kukamata soko katika maeneo
kadhaa.
Pia
ameitaka Bodi hiyo kuweka mkakati mahususi ya kukamata masoko mapya ya
watalii kutoka nje ya nchi kutoka nchi za Marekani, Hispania, Urusi na
nchi za Falme za Kiarabu zikiwemo za Dubai na Oman ambazo watu wake
wakiwemo wasomi, wafanyabiashara, wanamichezo na watu maarufu wanapenda
kwenda mapumziko ya muda mrefu na kutumia fedha nyingi kwa shughuli za
utalii.
Katika
hatua nyingine ameishauri Bodi hiyo kuwatumia watu maarufu na mashuhuri
wakiwemo wasanii na wanamichezo watakaoalikwa mahususi kwa kazi maalum
ya kutangaza utalii wa Tanzania.
“Licha
ya changamoto ya ufinyu wa bajeti tunaweza kuweka mikakati ya kutangaza
vivutio vyetu kwa tija na rahisi zaidi na kuifanya nchi yetu ijulikane
na kuonekana na watu wengi , kuna mikakati tunaweza kuifanya mara moja
tu ikadumu kwa muda mrefu, kama tukiwatumia watu mashuhuri wenye wafuasi
wengi wakatembelea vivutio vyetu tuna uhakika watu wengi zaidi
watafuatilia ziara zao na kufuata walichokichagua, lazima tuweke
mikakati ya kuwaleta watu mashuhuri walau 5 kwa mwaka ambao sisi
tutawaalika, tutapata mafanikio makubwa sana ndani ya muda mfupi”
Amesisitiza Dkt. Kigwangalla.
Kwa
upande wake Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constatine
Kanyasu akizungumza wakati wa uzinduzi wa Bodi hiyo amemshukuru Rais kwa
kuiongezea kipindi kingine cha miaka cha miaka 3.
Amesema
kuwa katika kipindi cha miaka 3 imefanya kazi kubwa licha ya changamoto
mbalimbali inazokabiliana nazo akisisitiza kwamba uwepo wa changamoto
hizo ni uhalali wa kuwepo kwa bodi hiyo.
Amesema
kuzinduliwa rasmi kwa bodi hiyo kutaifanya itekeleze majukumu yake kwa
kasi kubwa zaidi akisisitiza kwamba kupitia bodi hiyo sekta ya Utalii
Tanzania itasonga mbele kwa kasi kubwa zaidi.
Mhe.
Kanyasu ameitaka bodi hiyo iongeze juhudu ya kutangaza utalii na
kupanua wigo wa kutangaza soko la utalii ndani na nje ya nchi akisitiza
akisisitiza kwamba bado kuna mazao mengi ya utalii ambayo hayajavunwa na
endapo bodi itafanya kazi yake ipasavyo Tanzania itapata mafanikio
makubwa kiuchumi.
Naye
Mwenyekiti wa Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii Tanzania Jaji (Mst) Thomas
Mihayo akizungumza mara baada ya kuzinduliwa kwa Bodi hiyo amemshukuru
Rais hiyo nafasi nyingine akiahidi kwamba bodi yake itafanya kazi kwa
kasi na bidii zaidi ili kutimiza malengo ya kuitangaza Sekta ya utalii
ndani na nje ya nchi.
Jaji
Mihayo amesema kuwa Bodi hiyo itaendelea kutekeleza majukumu yake chini
ya uongozi wa Wizara na kuitangaza kikamilifu sekta ya utalii ndani na
nje ya nchi.
Bodi
hiyo yenye wajumbe 6 iliongezewa muda wa kuhudumu wa miaka 3 na Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli Aprili 23,
2019.
MWISHO.
No comments :
Post a Comment