Mwenyekiti
CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Kate Kamba akinywa maji ya moja ya kisima
cha Kimbiji na Mpera mapema leo mara baada ya kutembelea miradi ya maji
inayoendeshwa na Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA)
pamoja na kukagua maendeleo yake. Wa kwanza kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu
wa DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja na Katibu Mkuu Wizara ya Maji na
Umwagiliaji Profesa Kitila Mkumbo (mwenye tai nyekundu). Picha na
Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.
Katibu
Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji Profesa Kitila Mkumbo (kwanza kulia)
akitoa maelezo machache kwa kamati ya siasa ya mkoa wa Dar es Salaam.
Mkuu
wa Wilaya ya Kigamboni, Sarah Msafiri akimaliza kupokea kamati ya siasa
ya mkoa wa Dar es Salaam wakati wa ziara kukagua mradi ya DAWASA.
Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja akifafanua jambo.
Mjenzi
wa visima akitoa maelezo machache wakati wa ziara ya Kamati ya siasa ya
ya CCM Mkoa wa Dar es Salaam iliyoongozwa na Mwenyekiti CCM Mkoa wa Dar
es Salaam, Kate Kamba kutembelea miradi ya maji inayoendeshwa na
Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) pamoja na kukagua
maendeleo yake.
Mwenyekiti
CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Kate Kamba akizungumza na wafanyakazi wa
Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam (DAWASA) mapema leo Juni
4, 2019 wakati Kamati ya siasa ya ya CCM Mkoa wa Dar es Salaam
ilipotembelea maendeleo ya miradi yao mbali mbali.
Kamati ya siasa ya ya CCM Mkoa wa Dar es Salaam ikiwa pamoja na wafanyakazi wakisikiliza.
Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji Profesa Kitila Mkumbo akizungumza machache mbele ya wafanyakazi wa DAWASA.
Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja nae akieleza machache.
Bi. Peresi Msonya Mwakilishi wa Wafanyakazi akitoa shukrani.
Na
Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.
Wahandisi wa Maji nchini watakiwa kuwa wabunifu wa miradi
itakayoliwezesha taifa kuvuna na kuhifadhi maji ya mvua ili yatumike
kipindi kijacho.
Maji ya Mvua yamekuwa yakipotea hivyo wakiweza namna ya kuyaweka ili
yatumike baadae itasaidi kuvusha jamii pindi mito inapokauka.
Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dar es
Salaam, Kate Kamba wakati wa ziara ya Kamati ya siasa ya ya CCM Mkoa wa
Dar es salaam kutembelea miradi ya maji inayoendeshwa na Mamlaka ya
Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) pamoja na kukagua maendeleo
yake.
Amesema kuwa ifike wakati mamlaka zinazosimamia maji kuendelea kuwa
wabunifu katika uhifadhi maji.
Pia amewapongeza DAWASA kwa kusimamia na kufanikisha miradi mbalimbali
ya maji kwa fedha za ndani na kuacha kutengemea wafadhili kila kukicha.
"Jambo jema sana mnalolifanya nawaomba muendelee na moyo wa kujitoa na
kusimamia miradi yenu vyema mnayotumia fedha zenu za ndani, tena kwa
uaminifu wa hali ya juu," amesema.
Nae Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji Profesa Kitila Mkumbo
amewapongeza DAWASA kwa kuendelea kuamini na serikali kwa kusimamia
miradi mikubwa ya usimamizi wa maji Dar es Salaam.
Profesa Mkumbo amesema Serikali inaimani na nyie ndiyo maana miradi
mikubwa mnapewa ili ni jambo jema hivyo naomba usiiangushe na ikamilishe
kwa wakati.
Kwa upande wake Afisa Mtendaji Mkuu Mhandisi Cyprian Luhemeja amewaomba
wafanyakazi kuendelea kufanyakazi kwa bidii ili waweze kusimamia malengo
yao vyama.
Mhandisi Luhemeja amesema DAWASA ipo kamili kuendelea kuwapa maji wakazi
wa Dar es Salaam na Pwani ili kufikia lengo la usambazaji wa maji kwa
asilimia 95.
No comments :
Post a Comment