Mgeni
rasmi,katika mkutano Mkuu wa JATU,Ofisa Maendeleo ya Vijana kutoka
Ofisi ya Waziri Mkuu inayoshugulikia masuala ya ajira, Vijana na
walemavu, Eliachimu Mtawa akizungumza mbele ya wageni waalikwa katika
mkutano huo uliofanyika hivi karibuni jijini Dar
Mkurugenzi
wa Jatu PLC Peter Isare,akizungumza mbele ya Wageni waalikwa waliofika
kwenye mkutano huo,ambapo ameishukuru Serikali kwa ushirikiano na
kusisitiza kuwa kampuni hiyo ni ya umma kwani inawanachama zaidi ya
13,0000 na Agosti mwaka huu wataingia Soko la Hisa Dar es Salaam(DSE)
kwa mtaji wa Sh.bilioni 7.5.Pia akafafanua zaidi kwa wanachama wapya kuwa Kampuni hiyo ilianzishwa na vijana 2015 .
Pichani nyuma ni wajumbe wa bodi mpya ya Jatu PLC walioteuliwa kwenye mkutano huo na Wanachama wao.
Baadhi ya Wanachama wa Kampuni ya JATU wakifuatilia mkutano .
Mmoja
wa Wanachama wa JATU akiuliza swali kwa Uongozi wa kampuni hiyo akitaka
ufafanuzi wa baadhi ya jambo kuhusiana na MKutano huo. 

Picha ya pamojaSERIKALI
imeitaka bodi mpya ya Kampuni ya Jenga Afya Tokomeza Umaskini (Jatu
PLC), inafanya kazi kwa bidii na kuitendea vema dhamana waliyopewa.
Hayo
yamesemwa na Ofisa Maendeleo ya Vijana kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu
inayoshugulikia masuala ya ajira, Vijana na walemavu, Eliachimu Mtawa
ambapo
amesema anafurahi kuona Jatu hapa ilipofika kwani anaifahamu tangu mchakato wake wakati wanaanza.
amesema anafurahi kuona Jatu hapa ilipofika kwani anaifahamu tangu mchakato wake wakati wanaanza.
"Nakumbuka
walikuwa wakuja ofisini na maombio yao"Proposal), tunarekebisha,
tunawashauri, wanaenda wanarudi lakini mwisho tuliwasapoti na leo ni
kampuni kubwa, ofisi ya Waziri mkuu inajivunia katika hili,"amesema.
Ameongeza
kuwa dhamana ambayo wamepewa ni kubwa hivyo ameshauri wahakikishe
wanaitendea haki na Ofisi ya Waziri Mkuu kama walezi wa Jatu,
watafuatilia kwa karibu.
Mtawa
amesema mnyororo wa kilimo ni Mona ya juhudi zinazoweza badilisha
maisha ya mtu na kuwataka wasikubali kuyumbishwa na kurudi nyuma kwani
kuranya hivyo watakua wameikosea ofisi ya Waziri Mkuu na hata nafsi zao
zitawasuta.
Wakati
huo huo waliopitishwa kuwa wajumbe wa bodi mpya ya Jatu PLC ni Abdallah
Gonzi, ambaye ni Mwalimu wa Sheria Chuo Kikuu Cha Dar e s Salaam
(UDSM), Mhandisi Zakia Yona, Ian Semakande ambaye ni Mhasibu Finias
Upanga, Noel Kaganda na Mwajuma Hamza.
Awali,
akizungumza wakati akifungua mkutano huo Mkuu wa Wilaya ya Temeke
jijini Dar es Salaam Felix Lyaniva amesema Jatu inapoelekea soko la
hisa ni vema wakafuata Katiba yao na kuhakikisha hawapokei mnung'uniko
yeyote kutoka kwa wanachama.
"Kampuni
inaingia katika soko la hisa ni jambo zuri kwani mnaondoa umaskini
lakini hakikisheni hakuna manung'uniko, kupitia mkutano huu mkuu
wanachama kwa kauli moja tuseme tunataka kwenda huko katika soko la
hisa," amesema.
Lyaniva
amesema ni vema kukawa na uwazi na umakini katika masuala ya mapato na
matumizi ya jatu na yasomwe iwe wazi yanasomwa kwa utaratibu
waliojiwekea kwa mujibu wa Katiba.
"Mfate
katiba yenu inasema nini, mkae na kuzungumza vipaumbele vyenu pia
muweke uwazi katika masuala yenu kwa wanachama lazma menejimenti iwe
wazi kwa sababu mnatoka katika wazo moja kwenda lingine la kuingia
katika soko la hisa na sasa kampuni itakuwa sio ya mtu binafsi ni yenu
wote," amesisitiza.
Kwa
upande wake Mkurugenzi wa Jatu PLC Peter Isare, ameishukuru Serikali
kwa ushirikiano na kusisitiza kampuni hiyo ni ya umma kwani
inawanachama zaidi ya 13,0000 na Agosti mwaka huu wataingia Soko la Hisa
Dar es Salaam(DSE) kwa mtaji wa Sh.bilioni
7.5.
Akizungumzia
kampuni hiyo kwa wanachama wapya Isare amefafanua ilianzishwa na
vijana 2015 kuhusiana na masuala ya afya na lishe na haki za binadamu,
watu wengi wanapata changamoto kwenye masuala mbalimbali,
"wengi
ni maskini wanashindwa kumudu gharama za maisha na kusababisha migogoro
kwenye jamii,"alisema na kuongeza "Tuwe na afya lakini tuweze
kujitegemea na kuwa na afya nzuri, tumejikita kwenye kilimo, masoko na
bima ya afya, watu wengi wanahitaji kuwekeza katika biashara na
kuhitaji mikopo".
Pia
amesema kampuni hiyo ya umma imesajiliwa mwaka 2016 na imefanikiwa
katika kilimo cha mpunga Kilombero, Manyara kilimo cha alizeti na
Mahindi, Tanga kulimo cha Maharage.
"Tunawawezesha
wakulima kulima kilimo cha kisasa, na kuwapatia wataalamu ambao
watawapa elimu, na kilimo ni cha muda wote kisichotegemea hali ya hewa.
Igima kiwanda cha kukoboa mchele, Kibaigwa kiwanda cha mahindi na
alizeti, tunaunganisha kilimo na viwanda, na soko tumelitengeneza
wenyewe,"amesema.
Ameeleza
Jatu unaponunua chochote kama chakula, ni rahisi kukuza faida Kwani
kuna mfumo rasmi wa kugawa faida, mteja akinunua bidhaa anapata bonasi
ambapo gawio analipata mwisho wa mwezi.







No comments :
Post a Comment