
Aliyekuwa
Mkaguzi wa Ndani wa Kampuni ya Bia Tanzania(TBL), Richard Magongo,
amedai baadhi ya fedha zilizotolewa na TBL kwa Shirikisho la Mpira wa
Miguu (TFF) kwa ajili ya kudhamini timu ya Taifa ‘Taifa Stars’
zilitumika bila kuwa na nyaraka za uthibitisho wa matumizi.
Magongo
amedai hayo jana Juni 10 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele
ya Hakimu Mkazi, Maira Kasonde, wakati akitoa ushahidi kwa kuongozwa na
Wakili kutoka Takukuru, Leonard Swai.
Alidai
TBL iliingia katika mkataba na hilo wa kuidhamini Taifa Stars mwaka
2012 kwa miaka mitano ambapo jumla fedha za udhamini zilikuwa Dola za
Marekani, 10,000,000.
Shahidi
anadai walikuwa wakifanya ukaguzi wa fedha hizo kila inapofika robo
mwaka na taarifa za ukaguzi zilibainisha kwamba fedha za udhamini
zilitumika bila kuwa na nyaraka za kuthibitisha matumizi, kulikuwa na
matumizi ambayo hayakuwa ndani ya mkataba na mapungufu yalikuwa mengi
kiuhasibu na kiutawala kwa TFF katika utekelezaji wa mkataba.
“Matumizi
ambayo hayakuwa na nyaraka za uthibitisho ni mengi, mfano marejesho ya
mikopo kwa Jamal Malinzi hayakuwa na nyaraka za kuonyesha lini
aliikopesha TFF.
Washtakiwa
wengine katika kesi hiyo ni Mhasibu wa TFF, Nsiande Mwanga, Meneja wa
Ofisi TFF, Miriam Zayumba, Katibu wa shirikisho hilo, Selestine Mwesigwa
na Karani wa TFF, Flora Rauya ambao kwa pamoja wanakabiliwa na
mashitaka 30 katika kesi ya jinai namba 213 ya mwaka 2017.
Washtakiwa
wanakabiliwa na mashtaka mbalimbali yakiwamo ya kula njama, kughushi na
kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na utakatishaji wa dola za
Marekani 173,335.
Malinzi,
Mwesigwa na Nsiande wanaendelea kusota rumande kwa sababu wanakabiliwa
na mashtaka ya utakatishaji fedha ambayo hayana dhamana kwa mujibu wa
sheria.
No comments :
Post a Comment