
Spika
wa Bunge, Job Ndugai, ametoa wito kwa wabunge kuwekeza kwenye sekta ya
elimu badala ya magari aina ya Noah au pikipiki, akieleza kuwa wanamtia
aibu.
Wanafunzi
waliotambulishwa ni waliomaliza kidato cha nne mwaka 2018 katika Shule
ya Sekondari Sunshine na kupata ufaulu wa daraja la kwanza na pili.
"Pia
kuna wanafunzi 59 waliomaliza darasa la saba mwaka 2018 kutoka Shule ya
Msingi ya Anne Marie Academy ya jijini Dar es Salaam, kwenye wilaya,
hii shule ya ilikuwa ya kwanza na kimkoa ilikuwa ya kwanza na kitaifa
ilikuwa ya sita," alisema.
Kutokana na ufaulu huyo, Spika Ndugai alimpongeza Rweikiza ambaye ni mmiliki wa Shule ya Anne Marie kwa kuimarisha elimu.
"Haya
ndo mambo ambayo wabunge tunatakiwa tufanye, siyo mbunge unamiliki
Noah, unamtia aibu Spika, kila siku unaonekana trafiki huko, mbunge
unamiliki bodaboda!
"Tuvuke
jamani, bodaboda zikikamatwa, unampigia Spika, Spika bodaboda zangu
zimekamatwa huku," Ndugai alisema na kuibua vicheko bungeni.
Kiongozi
huyo wa Bunge alitoa rai kwa watunga sheria hao kuwekeza kwenye mambo
makubwa, akisema wanapaswa "kuvuka kidogo kwenye uwekezaji".
No comments :
Post a Comment