
Marekani
haijafurahishwa na vitisho vilivyotolewa na Waziri wa Mambo ya Nchi za
Kigeni wa Iran Mohammad Javad Zarif katika mkutano na mwenzake wa
Ujerumani Heiko Maas mjini Tehran.
Zarif
aliituhumu Marekani kwa kufanya vita vya kiuchumi kutokana na vikwazo
ilivyoiwekea Iran na akaonya kuwa wale wanaounga mkono vita wasitarajie
kuwa salama.
Maas anataka kuyaokoa makubaliano ya nyuklia na Iran, lakini hakupiga hatua zozote za maana wakati wa ziara yake nchini humo.
Maas alisema jana kuwa Ujerumani itafanya kila liwezekanalo kuhakikisha kuwa mvutano hauongezeki kati ya Marekani na Iran.
No comments :
Post a Comment