Serikali
imesema imeandaa mpango wa kutoa matibabu ya bure kwa watoto
watakaokuwa wakiugua ugonjwa wa Selimundu, kwa kupatiwa vibali maalum
vya huduma bila malipo kufuatia kufanyiwa uhakiki kwa familia
zisizojiweza.
Kauli
hiyo imetolewa leo Bungeni na Naibu Waziri wa Afya Maendeleo Jamii
Jinsia Wazee na Watoto, Dr Faustine Ndugulile, wakati akijibu swali la
Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Taska Mbogo, ambaye alihoji juu ya wagonjwa
hao kupewa matibabu ya bure.
Mbunge huyo amehoji kuwa "Serikali ina mpango gani kuwasaidia wagonjwa wa Sickle cell (Seli mundu) ili watibiwe bure?"
Akijibu
swali Naibu Waziri wa Afya Dr. Faustine Ndugulile amesema kuwa
"kupitia Wizara ya Afya tumeandaa muongozo wa kutoa msamaha kwa wagonjwa
wa Sickle cell (Seli mundu), familia zisizojiweza zitahakikiwa na
kupewa kibali cha huduma bila malipo. Serikali inaanzisha mpango wa
taifa kudhibiti magonjwa yasiyoambukiza."
No comments :
Post a Comment