Monday, June 10, 2019

Halima Mdee Aruhusiwa Kutoka Hospitali, Awashukuru Watanzania


Mbunge wa Kawe kupitia CHADEMA, Halima James Mdee, amewashukuru Watanzania kwa maombi yao pindi alipokuwa akiugua, huku akiwajulisha hali yake inavyoendelea kwa sasa.

Halima Mdee ameandika ujumbe huo kwenye ukurasa wake wa twitter na kusema kwamba hivi sasa amesharuhusiwa kutoka hospitali hivyo yupo nyumbani kwake, na anendelea vizuri kiafya.

Jumamosi ya Juni 9, zilitolewa taarifa kutoka kwa Mkurugenzi wa Itikadi, Mawasiliano na Uenezi wa CHADEMA, Bw. Joh Mrema, kuwa hali ya Halima Mdee haipo sawa kutokana na kufanyiwa upasuaji mkubwa wa kutolewa uvimbe tumboni.

No comments :

Post a Comment