Kamati
Kuu ya Chama ACT wazalendo kimemteua aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama Cha
Wananchi (CUF), Maalim Seif Shariff Hamad kuwa Mshauri Mkuu wa chama
hicho, ikiwa ni miezi michache tangu atangaze kujiunga na chama hicho.
Taarifa
iliyotolewa leo Jumatatu Juni 10, 2019 na Katibu wa Itikadi,
Mawasiliano na Uenezi, Ado Shaibu, kufuatia kikao cha kamati kuu ya ACT
Wazalendo kilichoketi Dar es Salaam jana Jumapili, imesema Maalim Seif
mwenye kadi namba moja ya chama hicho, ameteuliwa kuwa mshauri mkuu wa
chama.
Katika
nafasi za kamati kuu ya chama hicho, wafuasi wa Maalim Seif wameingizwa
akiwemo Fatma Fereji na Eddy Riyami, huku pia kukiwa na wajumbe wengine
waliongezwa ambao ni Theopista Kumwenda na Mwajabu Dhahabu.
Katika
nafasi za wenyeviti wa Kamati za Kitaifa, Nassor Marzurui ameteuliwa
kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Fedha na Miradi, huku Salim Bimani
akiteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Itikadi, Mawasiliano na Uenezi
na Joram Bashange akiteuliwa kuwa mwenyekiti wa kamati ya kampeni na
uchaguzi.
Wengine
ni pamoja na Ismail Jussa aliyeteuliwa kuwa mwenyekiti wa kamati ya
mikakati, usimamizi na ufuatiliaji, huku mbunge wa zamani wa viti
maalum. Mhonga Ruhwanya akiteuliwa kuwa mwenyekiti wa kamati ya
oganaizesheni, mafunzo na wanachama.
No comments :
Post a Comment