Kaimu Mkuu wa Idara ya Utawala na Rasilimali
Watu Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Stambuli Mapunda akizungumza na Wanafunzi
wa Kidato cha Nne Shule ya Sekondari Dodoma ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya
Wiki ya Utumishi wa Umma leo jijini Dodoma.
Mtakwimu Mkuu kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu
(NBS), Seif Kuchengo akiwasilisha mada kuhusu Sensa mbele ya Wanafunzi wa Kidato cha
Nne wa Shule ya Sekondari Dodoma ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya
Utumishi wa Umma leo jijini Dodoma.
Mwanafunzi wa Kidato cha Nne, Shule ya
Sekondari Dodoma, Bi. Najma Mussa akitoa neno la shukrani kwa niaba ya wenzake
mara baada ya kumalizika kwa mafunzo ya kuwajengea uelewa wa masuala ya Takwimu
yaliyoandaliwa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu(NBS) ikiwa ni sehemu ya maadhimisho
ya Wiki ya Utumishi wa Umma leo jijini Dodoma.
Baadhi ya Wanafunzi wa Kidato cha Nne Shule ya
Sekondari Dodoma wakifuatilia mada zilizokuwa zikiwasilishwa wakati wa mafunzo
ya kuwajengea uelewa kuhusu masuala ya Takwimu yaliyoandaliwa na Ofisi ya Taifa
ya Takwimu (NBS) ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma.
Baadhi ya Wanafunzi wa Kidato cha Nne Shule ya
Sekondari Dodoma wakiangalia vitabu walipotembelea Maktaba ya Ofisi ya Taifa ya
Takwimu (NBS) mara baada ya kumalizika kwa mafunzo ya kuwajengea uelewa wa
masuala ya Takwimu yaliyoandaliwa na NBS ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Wiki
ya Utumishi wa Umma leo jijini Dodoma. (Picha na: Frank Shija – MAELEZO)
No comments :
Post a Comment