Wednesday, June 19, 2019

MWILI WA MWANAFUNZI WA CHUO KIKUU CHA KAMPALA (KIU) ANIFA SIMPOLINUS WAAGWA DAR ES SALAAM, MASAUNI AONGOZA WAOMBOLEZAJI


MWILI wa mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Kampala (KIU), kampasi ya Gongolamboto jijini Dar es Salaam, Anifa Simpolianus C. Mgaya (22), umeagwa leo nyumbani kwao marehemu Mbezi SalaSala, jijini Dar es Salaam ambapo Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Mhandisi Yusuph Masauni na Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa walikuwa viongozi wa juu wa serikali waliohudhuria shughuli hiyo. Anifa aliuawamajira ya usiku  Juni 17, 2019 jirani kabisa na lango la kuingilia chuoni hapo na watu wanaosadikiwa kuwa vibaka. Tayari Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, limetangaza leo Juni 19, 2019 kuwa limemkamata kijana wa miaka 19, Ernest Joseph kwa tuhuma za mauaji hayo. Mwili wa marehemu umesafirishwa kwenda mkoani Iringa kwa mazishi 
Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam,Lazaro Mambosasa  akizungumza wakati wa ibada ya kumuaga  mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kampala, Anifa Simpoliunus, aliyefariki baada ya kuvamiwa na vibaka maeneo karibu na chuo hicho.Ibada hiyo imefanyika nyumbani kwa marehemu Mbezi SalaSala,jijini Dar es Salaam. Mwili wa marehemu umesafirishwa kwenda mkoani Iringa kwa mazishi
 Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akitoa heshima za mwisho mbele ya jeneza lililobeba mwili wa mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kampala, Anifa Simpoliunus, aliyefariki baada ya kuvamiwa na vibaka maeneo karibu na chuo hicho.Ibada ya kuaga mwili imefanyika nyumbani kwa marehemu Mbezi SalaSala,jijini Dar es Salaam. Mwili wa marehemu umesafirishwa kwenda mkoani Iringa kwa mazishi
 Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam,Lazaro Mambosasa  akitoa heshima za mwisho mbele ya jeneza lililobeba mwili wa mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kampala, Anifa Simpoliunus, aliyefariki baada ya kuvamiwa na vibaka maeneo karibu na chuo hicho.Ibada ya kuaga mwili imefanyika nyumbani kwa marehemu Mbezi SalaSala,jijini Dar es Salaam. Mwili wa marehemu umesafirishwa kwenda mkoani Iringa kwa mazishi
Waombolezaji wakimsikiliza Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(hayupo pichani)wakati wa ibada ya kuaga mwili wa  mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kampala, Anifa Simpoliunus, aliyefariki baada ya kuvamiwa na vibaka maeneo karibu na chuo hicho.Ibada hiyo  imefanyika nyumbani kwa marehemu Mbezi SalaSala,jijini Dar es Salaam. Mwili wa marehemu umesafirishwa kwenda mkoani Iringa kwa mazishi .(Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi).

No comments :

Post a Comment