Wednesday, June 19, 2019

BOT YATOA MUHTASARI WA TAMKO LA SERA YA FEDHA 2019/2020


Bank of Tanzania Logo Bank of Tanzania Logo


 
Utangulizi
Kwa mujibu wa Sheria ya Benki Kuu ya Tanzania, Sura ya 197, Benki Kuu inatoa Tamko la Sera ya Fedha linaloweka bayana mwelekeo wa...
sera ya fedha kwa mwaka 2019/20. Tamko hili linajumuisha mapitio ya mwenendo wa uchumi na utekelezaji wa sera ya fedha ya mwaka 2018/19, na kuainisha malengo ya sera ya fedha kwa mwaka 2019/20 yanayoendana na mahitaji ya malengo mapana ya kiuchumi ya Serikali ya kusimamia utulivu wa bei na ukuaji wa uchumi. Tamko hili pia linaelezea hatua  zinazokusudiwa kuchukuliwa na Benki Kuu ili kukia malengo hayo.

Mwenendo wa Uchumi wa Dunia
Kulingana na taarifa ya Mwelekeo wa Hali ya Uchumi wa Dunia iliyotolewa na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) mwezi Aprili 2019, uchumi wa dunia ulikua kwa wastani wa asilimia 3.6 mwaka 2018, ikilinganishwa na wastani wa asilimia 3.8 mwaka 2017. Ukuaji mdogo wa uchumi wa dunia ulichangiwa zaidi na athari za kiuchumi kutokana na majanga ya asili yaliyoikumba Japan, kuongezeka kwa vikwazo vya kibiashara baina ya Marekani na China, kudorora kwa upatikanaji wa rasilimali fedha, na kutokutabirika kwa athari za Uingereza kujitoa kwenye Umoja wa Kiuchumi wa Nchi za Ulaya.

Ukuaji wa uchumi wa nchi zilizoendelea ulikia asilimia 2.2 mwaka 2018, ukilinganishwa na ukuaji wa asilimia 2.4 kwa mwaka 2017. Hali hiyo ilichangiwa zaidi na kupungua uzalishaji wa magari nchini Ujerumani kutokana na kuanza matumizi ya sheria mpya za uchafuzi wa mazingira; kudorora kwa uwekezaji nchini Italia; na kupungua kwa matumizi ya  walaji nchini Ufaransa. Ukuaji wa uchumi nchini Uingereza ulipungua na kukia asilimia 1.4 kutoka asilimia 1.8, hasa kwa sababu ya hofu ya  kujitoa kutoka katika Jumuiya ya Ulaya (Brexit). Nchini Japan, ukuaji wa uchumi ulipungua hadi asilimia 0.8 kutoka asilimia 1.7, kutokana na kudorora kwa shughuli za kiuchumi katika robo ya tatu ya mwaka 2018, kulikosababishwa na hali mbaya ya hewa na maafa. Hata hivyo, ukuaji wa uchumi nchini Marekani umebakia kuwa imara, ukikua kwa asilimia 2.9 mwaka 2018, ikilinganishwa na asilimia 2.3 mwaka 2017, ingawa kumekuwa na kusuasua kwenye uwekezaji katika nusu ya pili ya mwaka 2018. Ukuaji wa uchumi wa nchi zinazoibukia kiuchumi na zile zinazoendelea  kukua ulikia asilimia 4.5 mwaka 2018 ukilinganishwa na asilimia 4.8  mwaka 2017. Ukuaji huu ulisababishwa na kudorora kwa masoko ya fedha katika nusu ya pili ya mwaka 2018. Ukuaji wa uchumi nchini China ulipungua hadi asilimia 6.6 mwaka 2018 kutoka asilimia 6.8 mwaka 2017, ukichangiwa zaidi na kupungua uwekezaji wa ndani, kupungua kwa mauzo ya magari pamoja na mvutano wa kibiashara na Marekani. Ukuaji wa uchumi nchini India ulikuwa asilimia 7.1 mwaka 2018, ukilinganishwa na asilimia 7.2 mwaka 2017. Ukuaji wa uchumi wa nchi za kusini mwa  jangwa la Sahara umeendelea kuimarika katika mwaka 2018, japo kwa kasi ya chini, huku wastani wa Pato Halisi la Taifa ukikadiriwa kukua kwa  asilimia 3.0 mwaka 2018, kutoka asilimia 2.8 iliyokiwa mwaka 2017.

Taarifa ya Mwelekeo wa Hali ya Uchumi wa Dunia iliyotolewa na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) mwezi Aprili 2019, inakadiria uchumi wa dunia utakua kwa asilimia 3.3 mwaka 2019, kutokana na matarajio ya ukuaji mdogo wa uchumi katika nchi zilizoendelea. Ukuaji wa uchumi wa mataifa yaliyoendelea unakadiriwa kupungua na kukia asilimia  1.8 mwaka 2019, kutokana na kuendelea kwa mvutano wa kibiashara baina ya China na Marekani, hofu ya nchi ya Uingereza kujitoa kutoka katika Jumuiya ya Ulaya (Brexit), na makadirio ya ukuaji mdogo wa uchumi wa nchi katika bara la Ulaya kutokana na kudorora kwa mahitaji ya sekta binafsi na uzalishaji viwandani. Ukuaji wa uchumi katika nchi zinazoibukia kiuchumi na zile zinazoendelea kukua, unatarajiwa kukua chini ya asilimia 5.0 mwaka 2019, kutokana na kupungua kwa ukuaji wa uchumi wa China, na kudorora kwa uchumi wa Uturuki na Iran. Wakati huo huo, inakadiriwa kuwa ukuaji wa uchumi wa nchi za kusini mwa Jangwa la Sahara, utaongezeka na kukia asilimia 3.5 mwaka 2019 kutoka  asilimia 3.0 mwaka 2018, kutokana na kuongezeka kwa kasi ya ukuaji uchumi kunakochangiwa zaidi na uwekezaji katika miundombinu. Viwango vya mfumuko wa bei katika nchi zilizoendelea na zile zinazoibukia kiuchumi vimeendelea kubaki katika viwango vya chini kutokana na kushuka kwa bei za chakula na nishati. Katika nchi za Jumuiya ya Afrika ya Mashariki (EAC), kasi ya mfumuko wa bei umeendelea kubakia katika kiwango kilichokubaliwa cha chini ya asilimia 8.0 kutokana na upatikanaji mzuri wa chakula. Katika nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa  Afrika (SADC), wastani wa mfumuko wa bei uliongezeka na kukia  asilimia 11.9 mwezi Aprili 2019 kutoka asilimia 8.5 mwezi Aprili 2018, ukichangiwa zaidi na kupanda kwa bei za chakula, mavazi na gharama za  usarishaji.

Kulingana na taarifa ya mwelekeo wa hali ya uchumi wa dunia iliyotolewa na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) ya mwezi Aprili 2019, viwango vya mfumuko wa bei katika nchi zilizoendelea unatarajiwa kupungua na kukia wastani wa asilimia 1.6 mwaka 2019, kutoka asilimia 2.0 mwaka  2018 kutokana na matarajio ya kupungua kwa bei za bidhaa. Wakati huohuo, mfumuko wa bei katika nchi zinazoibukia kiuchumi na zile  zinazoendelea kukua unatarajiwa kuongezeka kidogo hadi kukia wastani  wa asilimia 4.9 mwaka 2019, kutoka asilimia 4.8 mwaka 2018; kutokana na matarajio ya kuimarika kwa mahitaji nchini India na kupanda kwa bei za vyakula kwenye baadhi ya nchi.

Mwenendo wa Uchumi wa TanzaniaTanzania Bara
Uchumi wa Tanzania umeendelea kukua kwa kasi ya juu, ambapo kwa mwaka 2018 uchumi ulikua kwa wastani wa asilimia 7.0 ikilinganishwa na ukuaji wa asilimia 6.8 na asilimia 6.9 kwa mwaka 2017 na 2016, kwa mpangilio huo. Ukuaji huu umechochewa zaidi na uwekezaji katika huduma za kijamii na miundombinu, kutengemaa kwa ugavi wa umeme, hali nzuri ya hewa na utekelezaji wa sera ya fedha ya kuongeza ukwasi kwenye uchumi. Shughuli za kiuchumi zilizokua kwa kasi ya juu zaidi  ni pamoja na sanaa, burudani na starehe; ujenzi; usarishaji na uhifadhi;
sayansi na teknolojia; na mawasiliano. Shughuli za ujenzi zimeendelea kuwa na mchango mkubwa kwenye ukuaji wa uchumi zikifuatiwa na usarishaji na uhifadhi, mazao na viwanda. Uchumi unatarajiwa kukua  kwa asilimia 7.1 mwaka 2019, kufuatia uwekezaji unaoendelea katika kuboresha miundombinu na huduma za jamii, upatikanaji wa uhakika wa umeme, kuimarika kwa ukuaji wa mikopo kwa sekta binafsi, na uzalishaji

1 Kizio cha mwaka 2015
 
5
viwandani. Matarajio ya ukuaji wa juu wa uchumi yatatokana pia na maboresho yanayofanywa na serikali katika sheria na kanuni mbalimbali, mageuzi ya sera katika kujenga mazingira ya kuongeza uwazi katika kufanya biashara, pamoja na mkakati wa utekelezaji wa sera ya viwanda.Katika kipindi cha Julai 2018 mpaka Aprili 2019, mfumuko wa bei umeendelea kubakia ndani ya lengo la muda wa kati la asilimia 5.0, na ndani ya vigezo vya muunganiko wa kiuchumi katika Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) usiozidi asilimia 8.0, na wigo uliokubalika katika Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) wa kati ya asilimia 3.0 na 7.0. Hali hii ilichangiwa na kuongezeka kwa uzalishaji na upatikanaji wa chakula nchini, utekelezaji thabiti wa sera ya fedha na kibajeti, na kutengemaa kwa uzalishaji na ugavi wa umeme. Katika kipindi hicho, mfumuko wa bei ulikuwa wastani wa asilimia 3.2 ikilinganishwa na asilimia 4.5 katika kipindi kama hicho mwaka 2017/18. Aidha, mfumuko wa bei usiojumuisha bei za vyakula na nishati ulikuwa wastani wa asilimia 2.7 ukilinganishwa na asilimia 1.6. Mfumuko wa bei unatarajiwa kubakia ndani ya lengo la asilimia 5.0 katika mwaka 2019/20, kutokana na matarajio mazuri ya upatikanaji wa chakula cha kutosha, kuendelea kutengemaa kwa usambazaji wa umeme na utekelezaji thabiti wa sera ya fedha na kibajeti.Katika kipindi cha Julai 2018 mpaka Aprili 2019, mapato yaliyokusanywa na kuwekwa kwenye akaunti za Serikali zilizoko Benki Kuu ya Tanzania yalikuwa shilingi bilioni 14,690.4, ikiwa ni asilimia 3.4 zaidi ya mapato yaliyokusanywa na kuwekwa kwenye akaunti hizo katika kipindi kama hicho mwaka 2017/18. Kiasi hicho ni sawa na asilimia 93.1 ya makadirio ya makusanyo katika kipindi hicho. Mwenendo huu wa makusanyo ya mapato kwa sehemu kubwa umetokana na jitihada zinazotekelezwa na Serikali katika kuongeza matumizi ya teknolojia katika ukusanyaji wa kodi kupitia Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), na kuongezeka kwa  jitihada za usimamizi wa ukusanyaji wa mapato. Katika kipindi hicho,  jumla ya matumizi ya Serikali yaliyofanywa kupitia katika akaunti zake zilizoko Benki Kuu yalikia shilingi bilioni 16,363.6 kati ya hizo shughuli za maendeleo ziligharimu shilingi bilioni 4,864.6.Urari wa malipo nje ya nchi (balance of payments) ulikuwa na nakisi ya dola za Marekani milioni 1,089.2 katika kipindi cha Julai 2018 mpaka Aprili 2019, ikilinganishwa na ziada ya dola za Marekani milioni 299.2 katika kipindi kama hicho mwaka 2017/18. Hali hii ilichangiwa na kuongezeka kwa nakisi ya urari wa biashara ya bidhaa, huduma na uhamisho mali nchi za nje (current account decit). Nakisi ya urari wa biashara ya bidhaa,  huduma na uhamisho mali nchi za nje iliongezeka na kukia dola za Marekani milioni 2,132.6 ikilinganishwa na nakisi ya dola za Marekani milioni 1,709.5 katika kipindi kama hicho mwaka 2017/18 kufuatia kuongezeka kwa thamani ya bidhaa za mitaji zilizoagizwa kutoka nje ya nchi kwa ajili ya miradi mikubwa ya maendeleo, hasa ya miundombinu. Nakisi ya urari wa biashara ya bidhaa, huduma na uhamisho mali nchi za nje inatarajiwa kukia asilimia 4.4 ya Pato la Taifa mwaka 2018/19, kutoka asilimia 3.5 mwaka 2017/18.Akiba ya fedha za kigeni imeendelea kuwa ya kuridhisha na kuendelea kukidhi mahitaji ya fedha za kigeni kwa ajili ya kuagiza bidhaa na huduma kutoka nje ya nchi. Hadi kukia mwishoni mwa mwezi Aprili 2019, akiba ya fedha za kigeni ilikuwa dola za Marekani milioni 4,395.2, kutoka wa viashiria halisi vya ukwasi kwenye mabenki na hatimaye kusaidia usimamizi wa utekelezaji wa sera ya fedha na uhalisia wa riba katika masoko ya fedha. Wakati huo huo, Benki Kuu ipo katika hatua za mwisho za ukamilishaji wa mwongozo wa makubaliano ya uendeshaji wa soko la mikopo ya muda mfupi baina ya mabenki kwa kuweka dhamana (Global Master Repurchase Agreement ) ambao ni muhimu katika utekelezaji wa sera ya fedha.Ujazi wa fedha kwa tafsiri pana zaidi (M3) umeendelea kukua kwa wastani, wakati ukuaji wa mikopo kwa sekta binafsi ukiendelea kuimarika kwa kasi. Ukuaji wa mwaka wa ujazi wa fedha kwa tafsiri pana zaidi ulikia
asilimia 4.9 mwezi Aprili 2019 ambao ni chini ya lengo la asilimia 12.2 kwa mwaka unaoishia mwezi Juni 2019. Ukuaji huu wa fedha unaakisi ongezeko la matumizi ya kielektroniki katika kufanya malipo, hali ambayo imeongeza kasi ya mzunguko wa fedha katika shughuli za uchumi. Mikopo kwa sekta binafsi imeendelea kukua na kukia asilimia 10.6 mwezi Aprili 2019, kiwango ambacho ni cha juu kuwahi kutokea tangu mwezi Oktoba
2016 na juu ya lengo la ukuaji wa asilimia 10.2 ikapo Juni 2019. Ukuaji wa mikopo kwa sekta binafsi unaenda sambamba na muendelezo wa utekelezaji wa sera ya fedha inayolenga kuongeza ukwasi kwenye uchumi, pamoja na hatua zinazochukuliwa katika kupunguza mikopo chechefu kwenye benki za biashara kulikotokana na matumizi ya kanzi data ya taarifa za wakopaji katika kuidhinisha mikopo.Thamani ya shilingi ya Tanzania dhidi ya sarafu mbalimbali duniani imeendelea kuwa tulivu kwa kipindi chote cha kuanzia mwezi Julai 2018 mpaka Aprili 2019, japo kulikuwa na mabadiliko ya juu kiasi mwezi Januari na Februari 2019. Mabadiliko hayo yalitokana zaidi kwa kuwa kipindi hicho ni msimu wa mapato madogo yatokanayo na mauzo ya mazao nje ya nchi na shughuli za utalii, sambamba na ongezeko la uagizaji wa bidhaa za mitaji kutoka nje ya nchi kwa ajili ya miradi mikubwa ya maendeleo.

Matarajio ya Uchumi na Malengo ya Sera ya Fedha ya Mwaka 2019/20
Katika mwaka 2019/20, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar zitaendelea kutekeleza Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Miaka Mitano (Second Five Year Development Plan 2016/17 – 2020/21) na Mpango wa Kukuza Uchumi Zanzibar (MKUZA  III 2015-2020) zinazolenga kuendeleza jitihada za kuweka misingi imara ya uendelezaji wa viwanda na kukuza uchumi shirikishi kama hatua ya kuukisha uchumi wa nchi kuwa wa kipato cha kati. Katika mwaka 2019/20, Serikali zinalenga yafuatayo: i. Ukuaji wa Pato la Halisi Taifa la asilimia 7.1 kwa Tanzania Bara kwa mwaka 2019;ii. Mfumuko wa bei ulio ndani ya kiwango cha tarakimu moja; naiii. Nakisi ya bajeti ikijumuisha misaada kutoka nje (grants) ya asilimia 2.3 ya Pato la Taifa kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano kwa mwaka 2019/20.

Kwa upande wa Zanzibar, Pato la Taifa linatarajiwa kukua kwa asilimia 7.8 mwaka 2019, wakati nakisi ya bajeti ya serikali ya Zanzibar inatarajiwa kuwa asilimia 3.9 ya Pato la Taifa mwaka 2019/20.

Ili kukia malengo ya Serikali ya uchumi mpana kwa mwaka 2019/20, Benki Kuu ya Tanzania itaendelea kutekeleza sera ya fedha inayolenga  kuimarisha utulivu wa bei pamoja na utulivu wa riba katika masoko  ya fedha. Kwa mwaka 2019/20, Benki Kuu imepanga kukia malengo yafuatayo:i. Ukuaji wa wastani wa fedha taslim wa asilimia 9.0;ii. Ukuaji wa ujazi wa fedha kwa tafsiri pana zaidi (M3) wa asilimia 10.0;iii. Ukuaji wa mikopo kwa sekta binafsi wa asilimia 13.5; naiv. Kuwa na akiba ya fedha za kigeni inayotosha kuagiza bidhaa na huduma kutoka nje ya nchi kwa kipindi kisichopungua miezi minne.Katika utekelezaji wa majukumu yake, Benki Kuu itaendelea kuboresha ufanisi wa masoko ya fedha kuendana na mabadiliko ya utekelezaji wa sera ya fedha itakayotumia riba ya Benki Kuu. Vile vile, Benki Kuu itaendelea kutekeleza sera ya fedha kwa uwazi na kwa kutumia zana mbalimbali za sera ya fedha ili kuhakikisha kuwa kiasi cha ukwasi kwenye benki za biashara kinabakia katika kiwango kinachoendana na mahitaji ya wakati huo, na hivyo kuleta utulivu wa riba katika soko la fedha baina ya mabenki.

Hitimisho
Uchumi wa Tanzania unatarajia kuendelea kuwa imara kutokana na jitihada za Serikali katika kuendelea na uwekezaji katika huduma za jamii na miundombinu chini ya awamu ya Pili ya Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano na Mpango wa Kukuza Uchumi Zanzibar. Miradi inayotekelezwa katika mipango hii ni chachu katika kukuza sekta binafsi na kuwezesha uchumi wa viwanda. Kuendelea kuimarika kwa kasi ya ukuaji wa mikopo kwa sekta binafsi kutokana na utekelezaji wa sera ya fedha inayolenga kuongeza ukwasi katika uchumi, kuongezeka kwa uzalishaji viwandani pamoja na maboresho ya kanuni, sheria na sera zinazolenga mageuzi ya uchumi wa viwanda yatachangia katika ongezeko la Pato la Taifa katika mwaka 2019/20. Hata hivyo, athari zinazotokana na kuongezeka kwa vikwazo vya kibiashara baina ya mataifa makubwa duniani zinaweza kuathiri ukuaji wa uchumi wa Tanzania siku zijazo.Mfumuko wa bei unatarajiwa kubakia ndani ya lengo la muda wa kati la asilimia 5.0 kutokana na kuimarika kwa uzalishaji wa chakula; kuimarika upatikanaji wa nishati; na utekelezaji wa sera thabiti za fedha na kibajeti. Hata hivyo, kupanda kwa bei ya mafuta katika soko la dunia pamoja na hali ngumu ya upatikanaji rasilimali fedha katika soko la dunia kunaweza kuathiri thamani ya shilingi ya Tanzania na hivyo kusababisha mfumuko wa bei.Benki Kuu itaendelea kufuatilia kwa karibu mwenendo wa uchumi wa dunia na wa nchi katika kusimamia utekelezaji wa sera ya fedha inayolenga kudumisha utulivu wa mfumuko wa bei, na kuchukua hatua kulingana na uwiano wa sera na mikakati ya nchi katika kukuza uchumi. Hivyo, kutokana na tathmini ya mwelekeo wa uchumi wa dunia na uchumi wa ndani, pamoja na sera zinazotarajiwa kutekelezwa, ni matarajio ya Benki Kuu kuwa malengo ya sera ya fedha kwa mwaka 2019/20 yatakiwa.


No comments :

Post a Comment