Mtaalam
wa Tiba Radiolojia (Interventional Radiology) wa Hospitali ya Taifa
Muhimbili (MNH), Dkt. Erick Mbuguje (mwenye kofia ya bluu) na wenzake wa
MNH wakifuatilia jinsi mtaalam wa Tiba Radiolojia kutoka Marekani, Dkt.
Michelle Maneevese anavyomwekea mgonjwa wa figo mpira maalum kwenye
mshipa mkubwa wa damu (permanent catheter insertions) ambao unamsaidia
mgonjwa kusafisha damu (renal dialysis).
Wataalam
wa Tiba Raidolojia (Interventional Radiology) MNH wakiwa katika picha
ya pamoja na wataalam wa Tiba Ridolojia kutoka vyuo vikuu vya Emory na
Yale Marekani na hospitali iliyopo Buffalo New York. Wataalam hao kutoka
Marekani wanaongozwa na Dkt. Janice Newsome wa Chuo Kikuu cha Emory.
Daktari
Bingwa wa Tiba Radiolojia wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dkt.
Flora Lwakatare akizungumza na waandishi wa habari juu ya kuanzishwa kwa
huduma mpya ya kutibu uvimbe kwenye kizazi (uterine fibroids) kwa
kutumia njia ya kisasa ya Tiba Radiolojia (interventional radiology) na
kuweka mipira maalum kwenye mshipa mkubwa wa damu (permanent catheter
insertions) kwa wagonjwa wa figo ambao wapo kwenye mfumo wa kusafisha
damu (renal dialysis) au kwa wagonjwa wanaopatiwa tiba ya saratani.
Kushoto ni Daktari Bingwa wa Tiba Radiolojia kutoka Hospitali ya Chuo
Kikuu cha Emory nchini Marekani, Dkt. Dkt. Janice Newsome na Daktari
Bingwa wa Magonjwa ya Figo wa MNH, Dkt. Jonathan Mngumi.
Baadhi
ya wataalam wa MNH na Chuo Kikuu cha Yale na vyuo shiriki vya Emory na
Dartmouth) nchini Marekani wakimsikiliza Dkt. Lwakatare wa MNH.
Daktari
Bingwa wa Tiba Radiolojia kutoka Hospitali ya Chuo Kikuu cha Emory
nchini Marekani, Dkt. Janice Newsome akizungumza na waandishi wa habari
leo baada ya kutoa huduma ya tiba radiolojia kwa wagonjwa mbalimbali
nchini kwa kushirikiana na wataalam wa MNH. NA MWANDISHI WETU

Hospitali
ya Taifa Muhimbili (MNH) imeanzisha huduma mpya ya kutibu uvimbe
kwenye kizazi (uterine fibroids) kwa kutumia njia ya kisasa yaTiba
Radiolojia (interventional radiology) ambayo mgonjwa hatofanyiwa
upasuaji.
Pia
MNH imeanzisha huduma mpya nyingine ya kuweka mipira maalum kwenye
mshipa mkubwa wa damu (permanent catheter insertions) kwa wagonjwa wa
figo ambao wapo kwenye mfumo wa kusafisha damu (renal dialysis) au kwa
wagonjwa wanaopatiwa tiba ya saratani.
Wataalam
wa MNH kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Yale na vyuo shiriki (kama
Emory, Dartmouth) vya nchini Marekani wako kwenye programu maalum ya
mafunzo ya tiba Radiolojia tangu Octoba mwaka 2018 hospitalini hapa.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo, Daktari Bingwa wa Tiba Radiolojia wa MNH,
Dkt. Flora Lwakatare amesema mgonjwa mwenye uvimbe kwenye kizazi
anaingiziwa mpira wenye chembechembe maalum kwenye mishipa ya damu na
kwenda kuziba mishipa inayopeleka damu kwenye uvimbe.
“Baada
ya mishipa kuziba uvimbe unakosa damu au chakula chake na hivyo
kusinyaa na kufa kabisa. Hivyo basi mama mwenye uvimbe kwenye kizazi
endapo anapatiwa tiba hii hakuna haja ya kumfanyia upasuaji kubwa wa
kuondoa uvimbe,” amesema Dkt. Lwakatare.
Dkt
Lwakatare amesema faida ya kutumia njia hii ya kisasa, inamsaidia
mgonjwa kutofanyiwa upasuaji mkubwa na pia inampunguzia gharama za
matibabu na kuondoa hatari yoyote kwa mgonjwa aliyefanyiwa upasuaji
mkubwa.
Akizungumzia
huduma nyingine ya kuweka mipira maalum kwenye mshipa mkubwa wa damu
kwa wagonjwa wanaosumbuliwa na figo, Dkt Lwakatare amesema huduma hii
inawanufaisha wagonjwa wa figo ambao wako kwenye mfumo wa kusafisha damu
(renal dialysis) au wanaopatiwa tiba ya saratani.
Amesema
tiba hii inaondoa usumbufu wa kutumia mishipa midogo ya mikononi ambayo
mara nyingi ni ngumu kupatikana hasa kama inatumika mara kwa mara na
kwa muda mrefu.
“Tiba
hii inafaida kubwa kwa kuwa inawezesha kuepeuka upasuaji mkubwa ambao
una vihatarishi (risk), kuepeuka mgonjwa kukaa hopsitali kwa muda mrefu
na wanaofanyiwa tiba radiolojia mara nyingi wanaweza kurudi nyumbani
siku hiyo hiyo, hivyo inapunguza gharama kwa mgonjwa na Hospitali kwa
ujumla,” amesema.
Hivyo
kujengewa uwezo kwa watalaam wa ndani itasadia kwa kiwango kikubwa
kukuza huduma hii hapa nchini ambapo watalaam kutoka Hospitali za hapa
nchini watapata fursa ya kujifunza kwa gharama nafuu na kuongeza idadi
ya watoa huduma mikoani.
Naye
Daktari Bingwa wa Tiba Radiolojia wa Hospitali ya Chuo Kikuu cha Emory
nchini Marekani, Dkt. Janice Newsome amesema tiba radiolojia inahitaji
ubunifu na kutoa huduma kwa kushirikiana. Dkt. Janice Newsome amesema
wametoa mafunzo ya kutoa huduma ya tiba radiolojia kwa wataalam wa MNH
na kwamba wao wamejifunza mambo mbalimbali kupitia wataalam wetu.
“Kuwekeza
kwa wataalam ni jambo muhimu na zuri kwa kuwa kazi ya kutoa huduma
inahitaji kushirikiana,” amesema Dkt. Newsome. Katika mafunzo haya ya
awamu ya nne, wataalam 13 wa MNH wakiwamo madaktari, wauguzi na mafundi
sanifu wamepatiwa mafunzo sambamba na kutoa huduma ya matibabu kwa
wagonjwa mbalimbali.
Mafunzo
na huduma za tiba radiolojia zinazotolewa MNH ni mfululizo wa programu
mbalimbali za tiba radiolojia yayolianza Novemba 2017 ili kujenga uwezo
kwa wataalam wa MNH. Tangu kuanzishwa kwa huduma hii, wagonjwa 339
wamepatiwa huduma ya kibingwa ya tiba radiolojia na wengi ni wagonjwa
wenye uvimbe kinywani.

No comments :
Post a Comment