
Na WAMJW, Mwanza
SERIKALI
kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
imetenga Sh. bilioni tano katika mwaka wa fedha 2019/20 zitakazotumika
kujenga vituo vidogo vya uchangiaji damu salama katika mikoa 12 nchini.
Hayo
yameelezwa leo na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto, Ummy Mwalimu alipozungumza katika Maadhimisho ya Siku ya
Wachangia Damu Duniani yaliyofanyika kitaifa jijini Mwanza, viwanja vya
Furahisha. Sambamba
na hilo, Waziri Ummy amezindua mashine mpya ‘full automation’ za kupima
maambukizi katika damu na za kupima makundi ya damu ambapo mashine 24
zimesimikwa kwenye vituo vya kanda sita ikiwamo Dar es Salaam, Mwanza,
Tabora, Kilimanjaro, Mtwara na Mbeya.
Amesema
kila kituo kimesimikwa mashine nne ikiwa mbili ni za kupima magonjwa
yanayoambukizwa kupitia damu na mbili ni za kupima makundi ya damu.
Amesema
hatua hiyo imelenga kuimarisha huduma ya uchangiaji damu salama pamoja
na kuwezesha kusogeza karibu zaidi huduma za kuongezewa damu salama
wagonjwa wenye uhitaji.“Hadi
sasa kuna vituo vidogo vya damu salama nane ambavyo vimeanzishwa Mkoa
wa Dar es Salaam, Morogoro, Dodoma, Iringa, Kigoma, Shinyanga, Simiyu,
Tabora na Mara.
“Katika
mwaka wa fedha 2019/20, tunategemea kujenga vituo vya damu salama
katika mikoa 12, imetengwa Sh. bilioni tano, hivi karibuni ujenzi
utaanza,” amesema.Amesema
kadri huduma za matibabu ya kibingwa zinavyoboreshwa ikiwamo ya moyo
katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete, upandikizaji figo na upasuaji
mwengine Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI), Hospitali ya Taifa Muhimbili
na Mloganzila, zimepanua wigo wa mahitaji ya upatikanaji wa damu
salama.
“Jitihada
zinafanyika ili kuongeza wigo wa upatikanaji wa damu salama, kauli mbiu
ya mwaka huu inasema ‘Damu Salama kwa Wote’ ni kwa sababu mkutano mkuu
wa WHO mwaka huu ulihusu afya kwa wote.“Tunataka
kumfikia kila mtanzania mwenye mahitaji ya damu salama popote alipo
tuhakikishe anapata damu salama bila kikwazo chochote.
“WHO
inakadiria katika kila idadi ya watu 1000 zipatikane chupa 10 za damu,
Watanzania tunakadiriwa tupo milioni 55 tunapaswa kupata asilimia moja
ya idadi hiyo, hivyo chupa 550,000 zinahitajika kila mwaka kutosheleza
mahitaji,” amesema.Akitoa
ulinganisho amesema mwaka 2016 zilikusanywa chupa 196,000, mwaka 2017
chupa 233,000 na 2018 idadi imeongezeka kufikia chupa 307,000.
“Kumekuwa
na ongezeko la ukusanyaji damu, katika chupa 10 zinazohitajika
kupatikana angalau tunapata chupa sita, hivyo nawasihi watanzania wote
kujenga utamaduni wa kuchangia damu mara kwa mara ili tuweze kupata
inayotosheleza,” amesema.
Aidha,
amewataka waganga wakuu wa mikoa na wilaya kuhakikisha wanatekeleza
agizo alilowapa la kuandaa kambi za wazi kwa ajili ya uchangiaji damu
angalau mara tatu kila mwaka na watenge fedha katika bajeti zao
kuwezesha ukusanyaji damu salama.
Awali
akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mkuu wa Wilaya ya
Ilemela, Steven Lalika amesema walipewa lengo la kukusanya chupa 2000,
katika wiki ya uhamasishaji wamefanikiwa kukusanya chupa 3705 kufikia
Juni 13 na kwamba lengo la mkoa walikusudia kukusanya chupa 4000.
Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu
pamoja na viongozi wa kutoka Wizara ya Afya wakiongea na moja kati ya
watu waliojitokeza kuchangia damu, katika Maadhimisho ya Siku ya
Wachangia Damu Duniani yaliyofanyika kitaifa jijini Mwanza, viwanja vya
Furahisha.
opo
la watu waliojitokeza kushuhudia Maadhimisho ya Siku ya Wachangia Damu
Duniani yaliyofanyika kitaifa jijini Mwanza katika viwanja vya
Furahisha, yaliyofunguliwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu.
Baadhi
ya picha za Kikundi cha Wasanii wa filamu Tanzania wakionesha igizo
kuhusu uhamasishaji kwa jamii juu ya umuhimu wa kuchangia damu, tukio
limefanyika kitaifa jijini Mwanza katika viwanja vya Furahisha.







No comments :
Post a Comment