Hakimu katika Mahakama ya Wilaya ya
Otuke huko Uganda Kaskazini Alhamisi iliyopita aliachwa na mshangao
baada ya mtuhumiwa kuingia mahakamani hapo akiwa amevaa nguo zake
zilizoibiwa ambapo kufuatia
tukio hilo Hakimu alilazimika kuahirisha usikilizwaji wa kesi zote za
siku ile kwa wiki moja kwa ajili ya kuimarika kutokana na mshtuko
alioupata.
Imeelezwa kuwa mshukiwa huyo aliyeingia
mhakamani hapo aliachiwa huru na jaji Benjamin Seruru tarehe 24 Mei
baada ya kukutwa na hatia za kuiba mabegi, mtuhumiwa huyo Jimmy Oteng
(34) mkazi wa Okelo katika kijiji cha Amone alikutwa na hatia za kuiba
begi moja la ufuta kutoka nyumba moja huko Okelo mwaka 2018 na
akahukumiwa kifungo cha miezi 6 gerezani.
Hata hivyo Mei 24 hakimu Seruru aliamua kumwachia huru baada ya kushindwa kupatikana kwa baadhi ya ushahidi dhidi yake.
Siku moja baada ya kuachiwa kutoka jela
Oteng alifanya tukio la wizi nyumbani kwa hakimu huyo kwa kuiba suti
jozi nne na nguo nyingine pamoja na madumu mawili ya lita 20 aliyodhani
ni ya mafuta ya kupikia na alikamatwa siku ya jumatano wiki iliyopita.
Kamanda wa polisi wa Otuke alilieleza
gazeti la Daily Monitor kuwa mtuhumiwa huyo amewahi kuiba katika nyumba
mbili za watumishi wa mahakama ambao walieleza kuwa Oteng amewahi kuiba
mafuta ya kupikia pamoja na vifaa vingine vya nyumbani na baadaye kwenda
nyumbani kwa hakimu kufanya wizi huo.
Imeripotiwa kuwa Oteng amekuwa akifanya matukio hayo wakati mvua ikinyesha au wahusika wakiwa wameenda katika shughuli zao.
Imeelezwa kuwa baada ya kuiba katika
nyumba ya hakimu alikutwa na wawindaji wawili amejificha katika kichaka
huko Odugu katika kata ya Otuke ambao waliwaita polisi na akakamwatwa
akiwa na vitu mbalimbali vilivyoibiwa katika nyumba ya hakimu zikiwemo
suti jozi nne.
Kamanda wa polisi alieleza kuwa Oteng
alifikishwa mahakamani siku ya alhamisi ambapo hakimu Seruru alihairisha
kusikiliza kesi hiyo na kuamuru mtuhumiwa kubaki rumande hadi Juni 11
ambapo kesi hiyo itasikilizwa tena.
Na Leandra Gabriel, Blogu ya Jamii
No comments :
Post a Comment