Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab
Telack amefungua mkutano wa wadau wa huduma za afya ya uzazi na mtoto
kwa ajili ya kujadili Mapendekezo ya sheria ndogo za vijiji/halmashauri
za uboreshaji wa huduma za afya ya uzazi na mtoto katika halmashauri za
wilaya mkoa wa Shinyanga.
Mkutano huo uliolenga kujadili kwa
pamoja mikakati inayolenga kuboresha huduma za afya ya uzazi na mtoto
ili kuzuia vifo vitokanavyo na uzazi na vifo vya watoto
wachanga,umefanyika leo Jumatatu Juni 3,2019 katika ukumbi wa mikutano
wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga.
Telack alisema ili kuondoa vifo hivyo ni
vyema akina mama wajawazito wanahudhuria kliniki akibainisha kuwa pia
ni jukumu la baba kumhamasisha mkewe kuhudhuria kliniki na kujifungulia
kwenye vituo vya afya.
“Takwimu za mwaka 2018 zinaonesha kuwa
vifo vitokanavyo na uzazi mkoani Shinyanga vilipungua hadi 56 kutoka
vifo 73 mwaka 2017,vifo vya watoto wachanga vilipungua kutoka 915 mwaka
2017 hadi 913 mwaka 2018”,alieleza.
“Ingawa takwimu za vifo zinaonesha
kupungua.Nia ya serikali ni kuhakikisha mama mjamzito anajifungua salama
na mtoto wake anakua,Sote tutambue kuwa hakuna mama anayestahili kufa
wakati wa uzazi wala mtoto mchanga,hivyo ni lazima wadau wote tusongeze
jitihada,mikakati na rasilimali ili kuhakikisha tunakuwa na vifo
0”,aliongeza Telack.
Mkuu huyo wa mkoa alisema,Rasimu ya
mapendekezo ya uundwaji wa sheria ndogo za kuboresha afya ya uzazi na
mtoto imejumuisha mawazo kutoka kwa watendaji wa sekta ya afya ngazi za
halmashauri na kusititiza kuwa sheria ndogo zitakazoundwa zisikinzane na
Sheria mama,sera na miongozo katika sekta ya afya.
“Ninafurahi kuona kwamba moja ya mkakati
katika makubaliano yetu wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya ‘Jiongeze
Tuwavushe Salama’ unatekelezwa.Nawaelekeza wanasheria wa halmashauri na
Mwanasheria wa mkoa ambao pia ni washiriki wa mkutano huu kutumia weledi
wao kushauri na kuhakikisha kwamba kazi hii inakamilika kwa
wakati”,aliongeza.
Akiwasilisha rasimu ya sheria ndogo za
vijiji/halmashauri za uboreshaji wa huduma za afya ya uzazi na
mtoto,Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Dkt.Rashid Mfaume alivitaja
visababishi vinavyochangia vifo vya mama na mtoto kuwa ni kutokuhuduria
kliniki kwa wakati na mfumo dume unaosababisha mwanamke kutokuwa na
maamuzi.
Alisema sababu zingine kuwa ni
kutokufuata ushauri unaotolewa na wataalamu,mila na desturi potofu
pamoja na jamii kukosa elimu ya kutosha kuhusu dalili za hatari za
mjamzito,mzazi ana watoto wachanga.
ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab
Telack akifungua mkutano wa wadau wa huduma za afya ya uzazi na mtoto
ili kujadili Mapendekezo ya sheria ndogo za uboreshaji wa huduma za afya
ya uzazi na mtoto katika halmashauri za wilaya mkoa wa Shinyanga. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab
Telack akizungumza katika mkutano wa wadau wa huduma za afya ya uzazi na
mtoto.Kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Jasinta Mboneko,kulia ni
Katibu Tawala mkoa wa Shinyanga,Albert Msovela.
Katibu Tawala mkoa wa Shinyanga,Albert Msovela akizungumza wakati wa mkutano
wa wadau wa huduma za afya ya uzazi na mtoto ili kujadili Mapendekezo
ya sheria ndogo za uboreshaji wa huduma za afya ya uzazi na mtoto katika
halmashauri za wilaya mkoa wa Shinyanga.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Dkt.Rashid Mfaume akiwasilisha Mapendekezo/rasimu ya sheria ndogo za vijiji/halmashauri za uboreshaji wa huduma za afya ya uzazi na mtoto,Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Jasinta Mboneko akizungumza wakati wa mkutano
wa wadau wa huduma za afya ya uzazi na mtoto ili kujadili Mapendekezo
ya sheria ndogo za uboreshaji wa huduma za afya ya uzazi na mtoto katika
halmashauri za wilaya mkoa wa Shinyanga.
Mratibu wa Huduma za afya ya uzazi na
mtoto mkoa wa Shinyanga,Joyce Kondoro akitoa taarifa ya huduma za afya
ya mama na mtoto mkoa wa Shinyanga.
Katibu Tawala mkoa wa Shinyanga,Albert Msovela akiongoza majadiliano wakati wa mkutano
wa wadau wa huduma za afya ya uzazi na mtoto ili kujadili Mapendekezo
ya sheria ndogo za uboreshaji wa huduma za afya ya uzazi na mtoto katika
halmashauri za wilaya mkoa wa Shinyanga.
Wadau wa huduma za afya ya uzazi na mtoto wakiwa ukumbini.
Wadau wakiwa kwenye mkutano huo.
Wenyeviti wa halmashauri za wilaya wakiwa ukumbini.
Mkutano unaendelea.
Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Kishapu,Boniface Butondo akizungumza wakati wa mkutano huo.
Mkuu wa wilaya ya Kahama,Anamringi Macha akichangia hoja wakati wa mkutano huo.
Katibu Tawala Msaidizi Serikali za Mitaa Mkoa wa Shinyanga,Alphonce Kasanyi akitoa ufafanuzi kuhusu masuala ya sheria.
Mkurugenzi wa shirika la DSW, Peter Owaga akichangia hoja kwenye mkutano huo.
Mkurugenzi wa halmashauri ya Msalala Simon Berege akichangia hoja ukumbini.
Mkutano unaendelea.
Wadau wakiwa ukumbini.
Mkutano unaendelea.
Wadau wakiwa ukumbini.
Mkuu wa wilaya ya Kahama, Anamringi Macha akiwa ukumbini.
Mkutano unaendelea.
Katibu Tawala mkoa wa Shinyanga,Albert Msovela na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Dkt.Rashid Mfaume wakiteta jambo ukumbini.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
No comments :
Post a Comment