ASKOFU Mkuu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima
Dk.Josephat Gwajima ametinga Ikulu ambapo ametumia nafasi hiyo kueleza
wazi kwamba ili ule Chips Mayai ni lazima baadhi ya mayai yavunjike.
Ameeleza namna ambavyo anafurahishwa na
jitihada za Rais Dk.John Magufuli za kuleta maendeleo huku akitumia
nafasi hiyo kumshukuru kwa jitihada zake za ujenzi wa mradi wa kuzalisha
umeme katika Bonde la Mto Rufuji maarufu kwa jina la Stiegler.
Akizungumza leo Juni 3,2019 akiwa Ikulu
jijini Dar es Salaam, Askofu Dk.Gwajima amesema ni jambo nzuri kutoa
shukrani kwa Rais Dk.John Magufuli kwa jitihada zake za kuleta maendeleo
na hasa katika kuimarisha sekta ya nishati ya umeme.
"Kwanza ni jambo nzuri kuelewa ili ule
Chips Mayai lazima uvunje baadhi mayai. Kuna mayai lazima
yavunje.Namshukuru Rais kwa juhudi zake katika mradi wa umeme wa
Stiegler, mahala ambapo tutazalisha umeme mwingi tofauti na hapo zamani.
"Kumbuka wakati wa Mwalim Nyerere,wakati
wa Mwinyi, wakati wa Mkapa na wakati wa Jakaya Kikwete tulikuwa
tunazalisha umeme kiasi lakini kupitia .... tutazalisha umeme mwingi
kuliko Tanzania ilipoanzia,"amesema Askofu Gwajima.
Ameongeza kama ambavyo inafahamika watu
wengi wa nchi za Magharibi wanasema eneo hilo ni kwa ajili ya mazingira
pamoja na mambo mengine lakini ukweli hizo ni siasa za kimataifa.
"Kwa mfano ukiangalia miaka iliyopita
kulikuwa na mkataba kule Japani uliokuwa unafahamika Mkataba wa Kioto na
Marekani walikataa kusaini ule mkataba.Hivyo hata sisi tunatakiwa
kulinda Interest zetu,"amesema Askofu Gwajima.
Kuhusu ujumbe wake kwa Watanzania,Askofu
Gwajima amesema huu ni wakati wa kukimbia na si kutembea hivyo lazima
twende na kasi ya dunia."Dunia inakimbia hivyo lazima nasi Watanzania
tukimbie ili twende pamoja na dunia."
Habari na Said Mwishehe,Picha na Ikulu
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Askofu Mkuu wa
Kanisa la Ufufuo na Uzima Dkt. Josephat Gwajima Ikulu jijini Dar es
Salaam.
No comments :
Post a Comment