Na. Christopher Philemon, Monica Mutoni-Geneva.
Mkurugenzi
Mkuu wa Mamlaka Hali ya Hewa Tanzania (TMA) Dkt.Agnes Kijazi yupo
nchini Uswisi –Geneva kwenye Mkutano wa 18 wa Shirika la Hali ya Hewa
Duniani (WMO-18 Congress) .Mkutano huu hufanyika kila baada ya miaka 4
ambapo mwaka huu unafanyika jijiji Geneva kuanzia tarehe 3- 14 juni
,2019.
Katika
Mkutano huo utafanyika uchaguzi wa viongozi wakuu wa WMO ,ambao ni
pamoja na Rais ,Makamu wa Kwanza wa Rais ,Makamu wa Pili wa Rais ,Makamu
wa Tatu wa Rais na viongozi wengine wa Shirika la Hali ya Hewa
Duniani(WMO).
Tanzania
kupitia Dkt Agnes Kijazi amejitosa katika kinyang’anyiro cha kugombea
nafasi ya makamu wa tatu wa Rais wa WMO. Dkt Kijazi anaungwa mkono na
wakuu wote wa taasis za hali ya hewa barani Afrika na azimio hili
lilipitishwa katika Mkutano wa Mawaziri wenye Dhamana ya Huduma ya Hali
ya Hewa Barani Afrika (African Ministerial Conference on Meterology -
AMCOMET) tarehe18 - 23 Februari, 2019 Jijiji Cairo Misri ambapo
Tanzania iliwakilishwa na Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe.
Mhandisi Atashasta Nditiye ambaye kupitia hotuba yake alifanikiwa
kuwaombea wajumbe kumpitisha Dkt Kijazi kama mgombea pekee barani
Afrika.
“Kutokana
na umuhimu wa nafasi tunayoiomba kwa Taifa na Afrika kwa ujumla, na
hasa ukizingatia heshima ambayo tumepewa na Nchi za Afrika kuweka azimio
la kumuunga mkono Dkt Kijazi, ili achaguliwe katika nafasi ya makamu wa
tatu wa rais ambayo ina wagombea wengine kutoka mabara mengine, Wizara
ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kwa Kushirikiana Wizara ya Mambo ya
Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,zinazendelea kushiriki katika
kuomba wajumbe kutoka nchi mbalimbali hapa mjini Geneva kumpigia kura
Dkt.Kijazi ili ashinde nafasi hiyo” alisema Nditiye.
Tanzania
kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii iliandaa hafla ya kutangaza
vivutio vya utalii vinavyopatikana Tanzania kwa kuwaalika wajumbe
mbalimbali wa mkutano wa 18 wa WMO.
Aidha
katika salamu za viongozi wakuu wa WMO akiwepo Rais wa sasa wa WMO Bw
David Grimes aliwaomba wajumbe kumuunga mkono Dkt Kijazi kutokana na
uchapa kazi wake, kauli ambayo ilirudiwa pia na Katibu Mkuu wa WMO Prof.
Petteri Telaas alisema pamoja na utendaji uliotukuka wa Dkt Kijazi,
bado shirika hilo halijawahi kupata kiongozi kike kwenye nafasi ya juu
kama hiyo hivyo akawaomba pia wamuunge mkono.
MWISHO
No comments :
Post a Comment