Monday, June 10, 2019

Mbunge ahoji mpango wa Serikali kudhibiti wimbi la vijana kukimbilia mjini


Mbunge wa Viti Maalum, Fatma Toufiq (CCM) amehoji Serikali ina mpango gani wa kupunguza au kudhibiti wimbi la vijana wa vijijini kukimbilia mijini.

Akiuliza swali leo Bungeni Juni 10, Fatma amesema sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012 inaonesha kwamba asilimia 70 ya Watanzania wanaishi vijijini.

Amesema miaka ya hivi karibuni watu wengi hasa vijana wanakimbilia mijini huku wakidai kwamba maisha vijijini  ni magumu.

“Je, Serikali ina mpango gani wa kupunguza au kudhibiti hali hiyo?” amehoji Fatma.

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge,  Kazi, Ajira na Walemavu, Anthony Mavunde amesema ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM)  ya mwaka 2015-2020 imeelekeza Serikali kuboresha na kukuza uchumi wa vijijini ili kuongeza tija ya uzalishaji mali katika maeneo hayo kwa lengo la kuongeza fursa zaidi za ajira kwa vijana.

No comments :

Post a Comment