Mkuu wa Mafunzo na Mapambo wa Jeshi la Polisi Makao Makuu ya Dar es Salaam, Azizi Juma, anadaiwa kufariki dunia kwa kujinyonga.
Azizi
ambaye aliwahi kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja,
alikutwa ameshafariki dunia akiwa amening'inia katika mti wa mlimau
uliopo nyumbani kwake eneo la Kijichi.
Akithibitisha
kutokea kwa tukio hilo, Kamanda wa Polisi Zanzibar, Muhammed Hassan
Haji, alisema chanzo cha kifo hicho hakijajulikana.
“Alikutwa
amefariki dunia akiwa ananing'inia katika kitanzi kilichofungwa katika
mti wa mlimau uliopo nyumbani kwake Kijichi,” alisema.
Alisema kifo chake ni pigo na pengo kubwa kwa Jeshi la Polisi.
Aliitaka familia ya marehemu kuwa na moyo wa subira katika kipindi hiki kigumu cha msiba.
Juma
alizaliwa mwaka 1960 huko Michakaeni kijijini kwao kisiwani Pemba.
Alizikwa jana jioni katika makaburi ya Mwanakwerekwe mjini Zanzibar.
No comments :
Post a Comment