Uturuki imepewa ilani ya hadi mwisho wa mwezi Julai kuchagua kati ya kununua ndege za kivita za Marekani na makombora ya Urusi.
Kaimu
waziri wa ulinzi wa Marekani Patrick Shanahan ametoa ilani hiyo katika
waraka aliyomwandikia mwenzake wa Uturuki, Hulusi Akar.
Amesema Uturuki, haiwezi kumiliki ndege ya kisasa ya kivita chapa F-35 kutoka Marekani na makombora S-400 kutoka Urusi.
Washirika
hao wawili wa muungano wa kujihami kwa mataifa ya Magharibi Nato,
wamekuwa wakizozana kwa miezi kadhaa sasa kuhusiana na makombora ya
S-400.
Marekani
inahoji kuwa silaha hiyo ya Urusi haiambatani na mwongozo wa uundaji
silaha ya ulinzi uliyotolewa na Nato na kwamba ni tishio kwa usalama na
kuitaka Uturuki kununua ndege yake ya kivita badala ya makombora ''hatari'' ya Urusi.
Uturuki
ambayo imekuwa ikijikakamua kuimarisha ulinzi wake kwa kutumia sera
huru, imeagiza ndege 100 za kivita aina ya F-35 kutoka Marekani, na pia
imewekeza katika mpango wa F-35, huku kampuni zake zikitengeneza vipuri
937 ya sehemu ya ndege hizo.
Suala hili linaonekana kuwa msumari moto kwa mataifa yote mawili ya Uturuki na Marekani.
Akizungumza
katika kongamano la kila mwaka la Usalama Duniani, linalofahamikakama
Globsec Security Forum mjini Bratislava, Slovakia, Kamanda mkuu mpya wa
Nato, Generali Tod Wolters, aliisema "hatuna haja ya kushirikiana katika
uwezo wetu wa F-35 na Urusi".
Hii
ni wazi kuwa, Pentagon inaamini ikiwa Uturuki itaruhusiwa kununua ndege
yake ya kisasa ya kivita chap F-35 na pamoja na mtambo wa kisasa wa
kuzuia makombora ya S-400 mafundi wa Urusi wataweza kufikia mitambo ya
ndege hiyo hali ambayo itawaweka marubani wa Marekani katika hali ya
hatari.
Vikosi vya Marekanai, Uturuki na Urusi tayari vinafanya kazi katika eneo la kaskazi ni mwa Syria.
Lakini
mwanadiplomasia wa Uturuki wa ngazi ya juu -ambaye hakutaka jina lake
litajwe - ameniambia kuwa Washington ilipinga mpango wa Uturuki kununua
mtambo huo wa ulinzi kutoka Urusi baada yapande hizo mbili kutia saini
mkataba wa makubaliano.
Saa,
anasema,Uturuki haiwezi kujiondoa katika mkataba huo hata kama
ingelitaka kuchukua hatua hiyo . Uturuki ikitia saini mkataba, alisema,
inaheshimu mkataba huo.
Bw.
Shanahan alisma katika barua yake kuwa Marekani "imesikitika" kufahamu
kuwa maafisa wa Uturuki wametumwa Urusi kupewa mafunzo ya kuendesha
mtambo wa S-400.
"Uturuki
haitapokea ndege za F-35 ikiwa atanunua S-400," aliandika . "Bado mna
nafasi ya kuamua ikiwa mtabadilisha mawazo kuhusu ununuzi wa S-400."
"Hatutaki
F-35 ikaribiane na na makombora ya S-400 kwa muda kwasababu hawana
ufahamu wa kina kuhusu vifaa vilivyotumiwa kuunda silaha hiyo," Katibu
wa kudumu wa wizara ya Ulinzi Ellen Lord aliwaambia wanahabari.
Ndeg
enne za kwanza za F-35 ambazo zilikuwa ziwasilishwe kwa Uturuki bado
hazijaondoka rasmi Marekani ili kwawezesha marubani wa Uturuki kuanza
kujifunza nazo nchini humo.
Rais
wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan alisema siku ya Jumanne kuw ataifa lake
''limejitolea" kuendelea mbele na utekelezaji wa mkataba wa ununuzi wa
makombora ya S-400.
"Kwa
bahati mbaya hatukupokea mapendekezo yoyote kutoka Marekani kuhusiana
ununuzi wa silaha hii ya S-400 kutoka Urusi,"alisema .
Uturuki
ni taifa la pili lililo na wanajeshi wengi katika muungano wa Nato,
muungano wa kijeshi uliyo na wanachama 29- ambao ulibuniwa na mataifa ya
magharibu ili kujilinda zama za muungano wa Kisovieti.
Uhusiano kati ya Marekani na Urusi ulidorora kwa haraka baada ya Urusi kulimega eneo la Crimea kutoka Ukraine mwaka 2014.
Madai
ya Urusi kuingilia kati uchaguzi wa Marekani wa mwaka 2016 na kuhusika
kwake kijeshi nchini Sryria kuliongeza zaidi misukosuko.
S-400 ni mfumo wa aina gani?
S-400 au "Triumf" ni moja ya silaha ya hali ya juu duniani inayotoa ulinzi wa ardhini na angani.
S-400 moja ina uwezo wa kuangusha makombora 80 yaliyorushwa umbali wa kilomita 400 kwa wakati mmoja.
Urusi inasema kuwa ina uwezo kuangusha makombora yanayorushwa kutoka kwa ndege zisizo na rubani na makombora ya masafa marefu.
S-400 inafanya vipi kazi?
- Ni kifaa kilicho na uwezo wa kutoa taarifa kwa gari maalum inayoelekezwa katika eneo linalolengwa kushambuliwa
- Taarifa hizo zinatumwa kwa gari linalosaidia kurusha makombora na kuelekeza makombora angani
- Kifaa hiki pia kinasaidia kuelekeza makombora katika eneo maalum
No comments :
Post a Comment