Thursday, May 9, 2019

WATU WA MIJINI WATAKIWA KUBADILI MTINDO WA MAISHA ILI KUIMARISHA AFYA ZAO


IMG_20190509_080823
NA EMMANUEL MBATILO
Taasisi ya Chakula na lishe imewataka watu waishio mijini waweze kuboresha lishe zao ili waweze kuepukana na magonjwa yasiyoambukiza.
Akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam, mkurugenzi wa idara ya elimu na mafunzo ya lishe kutoka taasisi ya Lishe Bi. Sikitu Kihinga amesema kuwa ukiangalia data ambazo
zipo kwasasa inaonyesha kwamba ishu ya uzito uliozidi iko kubwa katika mijini ukilinganisha na sehemu ya mijini.
“Tumekutana hapa ili tuweze kuangalia ni mikakati gani tunaweza kufanya kwa pamoja ili kuhakikisha kwamba Lishe yetu inaimarika katika maeneo ya mijini”. Amesema Bi. Sikitu.
Aidha Bi. Sikitu ameongeza kuwa mtindo wa maisha tulionao kama vile kula vyakula vyenye mafuta yaliyozidi na kutokufanya mazoezi kusababisha kuzidi kwa uzito na magonjwa mbalimbali yasiyoambukiza.
“Watu wanaolisha watu mijini (Mama Lishe)  kuna vitu mbalimbali ambavyo tunaweza kuwasaidia kwasababu tunaona watu wengi wanaoishi mijini huwa hawana muda wa kuandaa vyakula hivyo kuwalazimu kwenda kwa mamalishe”. Ameongeza Bi. Sikitu.
Pamoja na hayo Bi. Sikitu amesema kuwa kukaa na mama Lishe waweze kuona ni mikakati gani wanaweza kufanya na kuwasaidia ili kwamba wanahakikisha wanafanya Lishe kwa watu wanaoishi mijini kuwa vizuri.
Kwa upande wa Afisa mipango wa Shirika la Global alience for improve Nutrition, Dkt. Winfrida Maila amesema  kuwa wanatakiwa kuweka mazingira mazuri kwa mama Lishe ili kuweza kuwashawishi watu wengi kupata chakula katika maeneo hayo.
“Chakula kinatakiwa kuwa katika makundi matano muhimu na si tu wanga kuwa mwingi, wanatakiwa watumie vyakula mchanganyiko”. Amesema Dkt. Winfrida

No comments :

Post a Comment