Na Woinde Shizza, Arusha
Wajasiriamali wadogo
wameiomba serikali kuwatafutia muwekezaji atakaewaletea mashine za
kutengeneza vifungashio pamoja na lebo ilikuweza kupunguza usumbufu wanaoupata.
kutengeneza vifungashio pamoja na lebo ilikuweza kupunguza usumbufu wanaoupata.
Iwapo tutapata
vifungashio bora na vizuri hitasaidia kukuza biashara yetu na kufanya
bidhaa zetu kuwa juu zenye ubora kitaifa na kimataifa zaidi.
Hayo yamebainishwa
Leo na mjasiriamali Annet Kivuyo alipokuwa akiongea Katika semina ya wajasiriamali iliandaliwa na shirika la uthibiti wa Viwango(TBS) kwa
kushirokiana na Sido ambapo alisema kuwa changamoto ya vifungashio
inachangia kwa kiasi kikubwa kupunguza soko la bidhaa za hapa nchini kwa
sababu vifungashio vyetu avipo kwenye ubora unao kubalika.
“vifungashio bora
vyakuvutia vitasaidia bidhaa zetu ziwe kwenye viwango vyenye ubora ,
serikali itushulikie tuwe na mtu atakae wekeza mashine za lebo na
kutengeneza vifungashio kama wenzetu wa nchi jirani kwani kwa sasa
tunaagiza nchi za nje na vinavyokuja pia vinakuwa vichache avitoshelezi
mahitaji “alisema annet
Alisema Tanzania tunabidhaa nzuri na vyenye ubora ila shida kubwa inayotusumbua ni
vifungashio hivyo aliitaji serikali ijitaidi kupata muekezaji atakae
saidia kuondoa tatizo Hili.
Kwa upande wake
mkurugenzi wa TBS Jabir Abdi alisema kuwa wameamua kufanya mafunzo haya
kwa wafanyabiashara wachakataji wa bidhaa za ngozi lakini pia huu ni
muendelezo wa kuhakikisha wanapata elimu sahihi itakayo wasaidia kufikia
viwango vya kitaifa ili waweze kuuza bidhaa zao sio tu hapa nchini
pia waweze kuuza nje ya nchi
Aidha alifafanua kuwa
wanatoa elimu hii pia ili waweze kupata alama za ubora pamoja na
kuwawezesha kufikia malengo yao, kitu pekee kitakachowawezesha
wajasiriamali kufikia malengo ni kufata sheria ya kufika viwango vya
kitaifa.
No comments :
Post a Comment