Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri
Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu
Mhe. Jenista Mhagama akizungumza wakati wa Mkutano wake na Viongozi wa
Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA) walipokutana kujadili
masuala ya Wafanyakazi nchini leo Aprili 26, 2019, katika ukumbi wa
PSSSF Jijini Dodoma. (Kushoto) ni Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt.
Phillip Mpango, (wa tatu kutoka kushoto) ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Selemani
Jaffo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora, Mhe. George Mkuchika na rais wa Shirikisho la Vyama vya
Wafanyakazi (TUCTA) Bw. Tumaini Nyamhokya.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe.
Dkt. Phillip Mpango akielezea jambo wakati wa mkutano huo, Kulia ni
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira
na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Mkuchika
(wa pili kutoka kulia) akisisitiza jambo kwa Viongozi wa Shirikisho la
Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA) walipokutana kujadili masuala ya
Wafanyakazi nchini leo Aprili 26, 2019, Jijini Dodoma. (Kushoto) ni
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Phillip Mpango na Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu)
Mhe. Jenista Mhagama na (wa tatu kutoka kushoto) ni Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe.
Selemani Jaffo.
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu
anayeshughulikia (Kazi, Vijana na Ajira) Mhe. Anthony Mavunde(wa kwanza
kushoto) pamoja na Katibu mkuu wa Ofisi hiyo Bw. Andrew Massawe
(katikati) na Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa
Umma na Utawala Bora, Dkt. Laurean Ndumbaro (wa kwanza kulia)
wakifuatilia mada wakati wa Mkutano huo.
Baadhi ya Viongozi wa Shirikisho
la Vyama Vya Wafanyakazi (TUCTA) wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye
Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama (hayupo pichani) wakati wa Mkutano huo.
Rais wa Shirikisho la Vyama vya
Wafanyakazi (TUCTA) Bw. Tumaini Nyamhokya akieleza jambo kuhusu masuala
ya Wafanyakazi nchini walipokutana Aprili 26, 2019 Jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu,
Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Bw. Andrew Massawe akichangia mada
wakati wa Mkutano huo walipokutana kujadili masuala ya wafanyakazi
nchini wakati wa kikao hiko kilichofanyika Jijini Dodoma.
Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Laurean Ndumbaro
akielezea jambo wakati wa Mkutano huo
Mwenyekiti Kamati ya Wanawake, Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Bi. Rehema Ludanga akichangia jambo wakati wa mkutano huo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri
Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu
Mhe. Jenista Mhagama (wa Pili kutoka Kushoto) wakiimba kwa pamoja na
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Phillip Mpango (Kushoto), (wa tatu
kutoka kushoto) ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Mkuchika na rais wa
Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA) Bw. Tumaini Nyamhokya.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri
Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu
Mhe. Jenista Mhagama (wa Pili kutoka Kushoto) akiwa kwenye picha ya
pamoja na Viongozi wa Shrikisho la Vyama vya Wafanyakazi mara baada ya
kumalizika kwa mkutano huo. (Kushoto) ni Waziri wa Fedha na Mipango Mhe.
Dkt. Phillip Mpango, (wa tatu kutoka kushoto) ni Rais wa Shirikisho la
Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA) Bw. Tumaini Nyamghokya, Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
George Mkuchika na Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA)
Bw. Tumaini Nyamhokya na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana
na Ajira) Mhe. Anthony Mavunde.
PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU
(KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU)
………………………..
Na. MWANDISHI WETU
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu anayeshughulikia Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye
Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama amewataka viongozi wa Shirikisho la Vyama
vya Wafanyakazi kuanzisha viwanda ili kuinua uchumi na kuchangia adhma
ya Serikali ya kuwa na uchumi wa viwanda.
Ametoa kauli hiyo hii leo Aprili
26, 2019 Jijini Dodoma wakati wa mkutano wake na viongozi hao
uliohudhuriwa na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango, Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora
Mhe. George Mkuchika, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Selemani Jafo pamoja na Naibu Waziri
anayeshughulikia Kazi, Ajira na Vijana Mhe. Anthony Mavunde ili kujadili
masuala yanayohusu wafanyakazi nchini.
Waziri mhagama aliwataka viongozi
hao kuwa wabunifu kwa kuanziasha viwanda vitakavyowezesha kujikwamua
kiuchumi pamoja na kuwajengea uwezo wa kujitegemea na kukuza mapato ya
vyama vyao.
“Niwaombe sana muwe na mitazamo
chanya katika kuchangia adhma ya Serikali kuwa na uchumi wa viwanda kwa
kuanzisha viwanda vitakavyowawezesha kukuza uchumi mfano viwanda vya
chaki, mbao na vingine vingi”, alieleza waziri Mhagama
Aidha aliwaeleza umuhimu wa
kuanzisha viwanda hivyo ikiwa ni pamoja na kuchangia ukuaji wa uchumi
nchini, kusaidia kuboresha maslahi ya wafanyakazi na kuongeza motisha na
kutoa fursa za ajira kwa wananchi kwa ujumla.
“Hii leo nimeona niwape changamoto
ya kuona umuhimu wa kuwa na viwanda vyenu kwa kuangalia mchango wenu
katika jamii na kuendelea kuwa na tija kwa kuzingatia umuhimu wa kuwa na
viwanda nchini,” alisisitiza Mhagama
Kwa upande wake rais wa Shirikisho
la Vyama vya Wafanyakazi nchini Bw. Tumaini Nyamhokya alishukuru
mchango wa serikali na maoni yao kwa kuwapa chachu ya kuona umuhimu wa
kuwa na viwanda na kuahidi kulifanyika kazi suala hilo.
“Kipekee nimefurahishwa na maoni
na mawazo ya serikali hivyo hatuna budi kuanza kulifanyia kazi suala
hilo ili kuendelea kuwa na mchango katika ukuaji wa uchumi wa nchi
yetu”, alisema Nyamhokya
Kwa upande wake Mwenyekiti wa
Kamati ya Wanawake Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA) Bi.
Rehema Ludanga alieleza alivyopokea ushauri huo wa serikali na kuona ni
namna bora ya kujishirikihsha katika uchumi wa viwanda na kuonesha
utayari wa kufanyia kazi suala hilo.
“Binafsi nikiwa kama mwenyekiti
Kamati ya Wanawake nimelichukua kwa dhati kabisa na nitajitahidi
kulifanyia kazi mapema iwezekanavyo ili wanawake nao waweze kunufaika na
fursa hii hasa upande wa sekta ya kilimo,” alieleza Bi. Rehema.
No comments :
Post a Comment