Wadau wa
Maendeleo mkoa wa Shinyanga wakiongozwa na Kampuni ya La Prince Pub
inayojihusisha na biashara ya uuzaji vinywaji na chakula Mjini Shinyanga
wamesherehekea Sikukuu ya Miaka 55 ya Muungano wa Tanganyika na
Zanzibar kwa kutembelea na kuwapatia misaada mbalimbali wagonjwa
waliolazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.
Miongoni
mwa zawadi zilizotolewa kwa akina mama na watoto ni pamoja na
sabuni,mafuta ya kujipaka juisi,poda, miswaki,dawa za meno,matunda,
toilet papers,biskuti,maji na zawadi zingine.
Wadau
walioungana na wafanyakazi wa La Prince Pub kutembelea na kutoa misaada
kwa wagonjwa leo Aprili 26,2019 ni pamoja na Kampuni ya Lulekia,Jambo
Food Products Co. Ltd,Astro Secure Co. Ltd,Uptown Holdings
Co.Ltd,Msirikale Microfinance,24 Security Tanzania,Ommy Fashion,
Gvenwear,Shirika la TVMC,Dellah Car Traders,Luxury Pub,Friends of Bhoke
na Malunde 1 blog.
Akizungumza
wakati wa kukabidhi zawadi hizo,Mkurugenzi wa Kampuni ya La Prince,
Athanas William alisema wameamua kuungana na wadau wa maendeleo mkoa wa
Shinyanga ikiwa ni sehemu ya kurudisha fadhila kwa jamii inayowazunguka.
Alisema
zawadi hizo kwa wagonjwa zimetolewa kupitia Mpango maalumu ulioanzishwa
na La Prince Pub unaojulikana kwa jina la ‘La Prince Charity Movement’
kwa lengo la kuisaidia jamii kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa
maendeleo yakiwemo mashirika yasiyo ya kiserikali,makampuni na
wafanyabiashara mbalimbali.
“Tumefika
hapa katika hospitali ya mkoa wa Shinyanga kwa ajili ya kutoa pole kwa
wagonjwa na kuwapa misaada mbalimbali,tumejumuika sisi wafanyakazi wa La
Prince na wadau wengine wa maendeleo wakiwemo kutoka kwenye mashirika
na makampuni ambao tumeungana kuja kurudi kurudisha fadhila kwa jamii
kwa kutoa misaada kwa wagonjwa katika wodi za akina mama na
watoto”,alisema.
“Tukiwa
sehemu ya jamii tumeona ni busara zaidi katika siku hii ya kuadhimisha
miaka 55 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ambayo hatufanyi sherehe
za kitaifa,sisi tumeona tufanye sherehe ndogo ya kuwapa pole wanaoumwa
na wenye mahitaji maalumu”,aliongeza William.
“Kilichotusukuma
sisi ni moyo wa upendo,sisi tuna mpango maalumu unaitwa La Prince
Movement ambapo kila mwezi tumeamua kuunganisha wadau mbalimbali wa mkoa
wa Shinyanga kutoa misaada mbalimbali katika kada mbalimbali, leo
tumeanza na hospitali na hivi karibuni tutambelea magereza”,alieleza Mkurugenzi wa La Prince Pub.
ANGALIA PICHA HAPA
Mkurugenzi wa Kampuni ya La Prince,
Athanas William akizungumza katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa
Shinyanga wakati wadau mbalimbali wa maendeleo walipotembelea wagonjwa
na kuwapatia zawadi akina mama na watoto waliolazwa katika hospitali
hiyo leo Aprili 26,2019 ikiwa ni siku ya maadhimisho ya miaka 55 ya
Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Picha zote na Kadama Malunde – Malunde1 blog
Mmoja wa
wafanyakazi wa La Prince Pub akiweka sawa zawadi mbalimbali zilizotolewa
na wadau wa maendeleo mkoa wa Shinyanga kwa ajili ya akina mama na
watoto waliolazwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga.
Baadhi ya wafanyakazi wa La Prince Pub wakiwa wamebeba zawadi mbalimbali.
Wadau wa maendeleo wakiwa na zawadi
zao wakijiandaa kuingia katika wodi mbalimbali katika hospitali ya rufaa
mkoa wa Shinyanga kwa ajili ya kugawa zawadi hizo kwa wagonjwa.
Wadau wa maendeleo wakielekea katika wodi za watoto.
Mkurugenzi wa Kampuni ya La Prince,
Athanas William akizungumza katika moja ya wodi akielezea lengo la wadau
kufika katika hospitali hiyo.
Wadau wa maendeleo wakiwa wodini na zawadi zao kabla ya kuanza kuzigawa.
Mkurugenzi
wa Kampuni ya La Prince, Athanas William akisalimiana na mmoja wa
Madaktari katika hospitali ya rufaa mkoa wa Shinyanga aliyekutwa wodini.
Wadau wakitoa zawadi kwa mama aliyelazwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga.
Mkurugenzi wa Kampuni ya La Prince, Athanas William akizungumza katika moja ya wodi za akina mama.
Wafanyakazi wa Ommy Fashion wakitoa zawadi kwa mgonjwa.
Wafanyakazi wa La Prince Pub wakitoa zawadi katika wodi ya watoto.
Mkurugenzi wa Kampuni ya La Prince, Athanas William akisalimia akina mama katika wodi ya watoto.
Utoaji zawadi ukiendelea katika wodi ya akina mama waliojifungua. katikati ni Bhoke Wambura, muanzilishi wa Friends of Bhoke.
Wadau
wakiongozwa na Mkurugenzi wa shirika la TVMC,Musa Jonas Ngangala
(katikati) wakikabidhi zawadi ya ndoo ya sabuni na zawadi zingine kwa
mama aliyejifungua watoto mapacha wa kiume.
Wafanyakazi
wa La Prince wakimsalimia na kumpa pole pamoja na zawadi mama wa mmoja
mfanyakazi mwenzao aliyelazwa katika wodi ya wanawake.
Picha zote na Kadama Malunde – Malunde1 blog
No comments :
Post a Comment