Daktari bingwa wa magonjwa ya
moyo kwa watoto wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Godfrey Mbawala
akizungumza na madaktari bingwa wa magonjwa ya moyo kutoka Hospitali
kuu ya jimbo la Shandong la nchini China walipotembelea taasisi hiyo leo
Jijini Dar es Salaam.
Daktari wa magonjwa ya moyo kwa
watoto kutoka Hospitali kuu ya jimbo la Shandong la nchini China
anayejitolea katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Zhao Lijian
akiwaelezea madaktari wenzake kutoka China namna ambavyo anatoa huduma
ya matibabu ya moyo kwa watoto walipotembelea taasisi hiyo leo Jijini
Dar es Salaam
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya
Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akizungumza na
madaktari bingwa wa magonjwa ya moyo kutoka Hospitali kuu ya jimbo la
Shandong la nchini China walipotembelea taasisi hiyo na kuahidi
kushirikiana na taasisi hiyo kuboresha sekta ya afya ikiwemo afya ya
moyo leo Jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya
Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi (katikati) akipokea
zawadi ya picha ya Shandong kutoka kwa kiongozi wa madaktari bingwa wa
magonjwa ya moyo kutoka Hospitali kuu ya jimbo la Shandong la nchini
China Wang Zhifeng walipotembelea taasisi hiyo leo Jijini Dar es Salaam
na kuahidi kuendelea kushirikiana na taasisi hiyo katika kubadilishana
ujuzi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya
Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi katika picha ya pamoja
na menejimenti ya taasisi hiyo na madaktari bingwa wa magonjwa ya moyo
kutoka Hospitali kuu ya jimbo la Shandong la nchini China walipotembelea
taasisi hiyo na kuahidi kuendeleza ushirikiano katika sekta ya afya
ikiwemo magonjwa ya moyo leo Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya
Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akifafanua jambo
alipokua akizungumza na madaktari bingwa wa magonjwa ya moyo kutoka
Hospitali kuu ya jimbo la Shandong la nchini China walipotembelea
taasisi hiyo na kuahidi kuendeleza ushirikiano katika kutoa huduma za
matibabu ya moyo leo Jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi wa Kurugenzi ya
Upasuaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Angela Muhozya
akielezea namna idara ya upasuaji inavyofanya kazi alipokua akizungumza
na baadhi ya madaktari bingwa wa magonjwa ya moyo kutoka Hospitali kuu
ya jimbo la Shandong la nchini China walipotembelea taasisi hiyo leo
Jijini Dar es Salaam.
………………………………………………………………………………………………
Na Zawadi Masinde – JKCI
Madaktari
bingwa wa magonjwa ya moyo kutoka Hospitali kuu ya jimbo la Shandong
nchini China wanatarajia kuja nchini mwezi wa nane mwaka huu kwa ajili
ya kufanya kambi maalum ya
matibabu ya moyo katika Taasisi ya Moyo
Jakaya Kikwete (JKCI).
Makubaliano
hayo yamefikiwa leo katika kikao cha pamoja cha viongozi kutoka
Hospitali hiyo na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete kilichofanyika jijini
Dar es Salaam.
Akizungumza
katika kikao hicho Kiongozi wa msafara huo Wang Zhifeng alisema
wataalamu hao ambao watakuja nchini watafanya upasuaji wa moyo wa
kufungua na bila kufungua kifua pia watabadilishana ujuzi wa kazi na wenzao wa JKCI.
“Wataalamu wetu kutoka Hospitali ya Shandong wakija
hapa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete watakuja na vifaa tiba ambavyo
watavitumia katika upasuaji watakaoufanya. Pia mtatuambia ni vifaa gani
vingine ambavyo mnavihitaji ili wataalamu wetu watakapokuja waje navyo”,
alisema Zhifeng .
Aliendelea kusema kuwa
kabla ya kuja kwa wataalamu hao hapa nchini kutaanza na program ya
madaktari, wauguzi, wataalamu wa usingizi, mafundi sanifu wa moyo na Wahandisi wa vifaa tiba kwenda katika Hospitali hiyo kwa ajili ya mafunzo ya muda mfupi ya magonjwa ya moyo na mashine za moyo.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI Prof. Mohamed Janabi aliwashukuru viongozi hao kwa kutembelea Taasisi hiyo na kusema kuwa kuja kwa wataalamu hao ni matokeo ya mkataba wa mahusiano uliosainiwa mwezi wa nane mwaka jana.
Makubaliano yaliyosainiwa katika mkataba huo ni kutolewa kwa mafunzo ya muda mfupi
kwa madaktari, wauguzi, mafundi sanifu wa moyo na wahandisi wa vifaa
tiba, kujenga jengo jipya la Taasisi hiyo, kutoa msaada wa vifaa tiba na kufanya kambi maalum za matibabu ya moyo ambazo zitasaidia kuwajengea uwezo wataalam wa hapa nchini.
Naye
Mratibu wa ushirikiano wa Tanzania na China katika sekta ya Afya Dkt.
Ligile Vumilia alisema makubaliano yaliyofikiwa katika kikao hicho ni
lazima yafanyike kwa wakati na kwa manufaa ya nchi kwani hakuna Taasisi
itakayotoa matibabu ya moyo zaidi ya wataalamu waliopo katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete.
Hospitali kuu ya jimbo
la Shandong inautaalamu wa hali ya juu wa kutibu magonjwa ya moyo ikiwa
ni pamoja na kufanya upasuaji wa kufungua na bila kufungua kifua ambapo
kwa mwaka 2018 ilifanya upasuaji wa moyo kwa wagonjwa 85,000.
No comments :
Post a Comment