Mmoja waandaaji wa ripoti hizo
Bi. Pili Mtambalike akifafanua kuhusu ripoti ambayo ameiandaa kwaajili
ya waandishi wa habari katika hafla iliyofanyika kwenye ukumbi wa
Kizenga Milenium Tower Makumbusho.
……………………………………………………………………………………………….
NA EMMANUEL MBATILO
Baraza la Habari
Tanzania (MCT) limewataka waandishi pamoja na wahariri hapa nchini
waweze kuwa makini katika uandaaji wa taarifa ambazo zinakidhi kiwango
na zenye maadili ya uandishi na pia zisiegemee upande mmoja kwani
kunaweza kumsababishia kuingia kwenye wakati mgumu.
Hayo yamesemwa leo
katika uzinduzi wa machapisho ya vitabu ambavyo vimetoa ripoti
mbalimbali juu ya uhuru wa wanahabari katika vyombo vya habari hapa
nchini hasa kutokana na matukio mbalimbali yaliyojitokeza hivi karibu
ikiwemo kupotea kwa waandishi na wengine kutishiwa.
Akizungumza na
wanahabari jijini Dar es Salaam, Jaji Mstaafu Juxon Mlay amesema kuwa
tunalinda na kutetea uhuru wa wanahabari kwaajili ya wananchi kupata
habari na si kwaajili ya wanahabari pekee.
“Mazingira ya sasa ni
magumu katika tasnia ya uandishi wa habari, sasa yale ambayo yameandikwa
kwa kutuonya, kutuelekeza na kutukumbusha humu ni muhimu kwetu ili
tuweze kufanya kazi kwa ufanisi zaidi katika mazingira ya sasa wakati
huohuo tukiwa tukijalibu kupambana na kushirikiana na wale wenye mamlaka
ili kuboresha haya mazingira ya kufanya kazi zetu”. Amesema Bw.Mlay.
Kwa upande wa mwandishi
wa chapisho la taarifa inayomhusu mwandishi wa Channel Ten Geofrey
Nilahi ambaye alikuwa Ruvuma, Bw. Attilio Tagalile amesema kuwa mwaka
jana mwandishi huyo aliwaandikia viongozi wa MCT ya kuwa maisha yake
yapo hatarini kutokana na kazi ambayo anaifanya hasa kutokana na kutoa
taarifa ambayo ilikuwa inamkwaruzano baina ya wananchi na serikali.
“Alikuwa ameandika
taarifa za kichunguzi zilikuwa zinaonyesha matatizo yaliyokuwa katika
maeneo yale ambapo matatizo hayo ni pamoja na matatizo ya shule kutokana
na wanafunzi kusoma katika mazingira magumu ikiwa jimbo hilo lina
viongozi wakubwa”. Amesema Tagalile.
“Yeye anavyodai ni
kwamba baada ya kupata stori zake alijaribu kupata wahusika ili aweze
kubalansi stori zake kwamaana ya wabunge pamoja na wakuu wa wilaya na
vilevile. Mbuge wa jimbo la Peramiho Jenista Mhagama alitumiwa ujumbe
mara mbili lakini hakujibiwa”. Ameongeza Tagalile.
Hata hivyo Bw. Tagalile
amesema kuwa waandishi walishiriki kufuta ile taarifa ambayo
ameiandika
mwandishi Nilahi, waandishi ambao walikuwa wanatakiwa kumuunga mkono
kwa harakati zake lakini chakushangaza wao ndo wanakuwa chanzo cha
kumkandamiza mwenzao.
Kwa upande wa Bi. Pili
Mtambalike amesema ripoti ambayo ameia imelandaa imelenga kuangalia
changamoto mbalimbali ambazo vyombo vya habari vimepitia ikiwemo masuala
ya sheria,masuala ya sera za nchi pamoja na changamoto mbalimbali
zitokanazo na sheria za vyombo vya habari.
“Hivi karibuni gazeti
la Citizen lilifungiwa baada ya kuandika masuala ya uchumi, masuala ya
uchumi si rahisi kukosewakosewa kwasababu kuna wachumi waliobobea ambao
unaweza kuwauliza pia kuna takwimu zinatolewa na benki kuu pamoja na
wizara husika na kama ni mwandishi mzuri ukiziandika zile huwezi kuwa na
mashaka na taarifa yako”. Ameongeza Bi. Pili.
Aidha kwa upande wa Bw.
Absalom Kibanda amesema kuwa katika chapisho la ripoti ambalo
ameliandaa limelenga kuwakumbusha wanahabari wajibu wao kitaaluma pamoja
na kimaadili ambapo hali ya vyombo vya habari kwasasa kuna wasomi wengi
kuliko zamani.
“Kwanini kuna kuwa na
ukiukwaji wa kitaaluma pamoja na misingi ya kimaadili kuliko ilivyokuwa
zamani ambapo wasomi walikuwa wachache na pengine hili kwasisi katika
vyombo vya habari tunatakiwa tujitathimini kama tutatimiza wajibu wetu
kitaaluma na vilevile kimaadili”. Amesema Kibanda.
No comments :
Post a Comment