Mhe. Waziri wa Elimu, Sayansi,
Teknolojia na Ufundi Profesa Joyce Ndalichako akiweka saini kwenye
kitabu cha wageni kwenye eneo la ujenzi wa Jengo la Taaluma na Utawala
la chuo Kikuu Mzumbe Kampasi ya mbeya mara tu baada ya kuwasili.
Aliyeshika kitabu ni Injiani Thadeus Koyanga na kushoto anayeshuhudia
tukio hilo ni Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Profesa Lughano Kusiluka (
Mwenye Kaunda suti kushoto)
Mhe. Waziri wa Elimu, Sayansi,
Teknolojia na Ufundi Profesa Joyce Ndalichako (kushoto) akiwa na Makamu
Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Profesa Lughano Kusiluka ( Mwenye Kaunda suti
kushoto) pamoja na Mkandararasi na wajenzi; wakikagua ramani ya jengo
la Taaluma na Utawala la Chuo Kikuu Mzumbe Kampasi ya Mbeya.
Mhe. Profesa Ndalichako (katIkati)
akikagua mahali litakapojengwa jiwe la msingi ambalo litawekwa rasmi
na Mhe. Rais wa Jamhuri wa Muuungano wa Tanzania Dr.John Pombe Joseph
Magufuli Mei 1, 2019. Kushoto ni Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe
Profesa Lughano Kusiluka na kulia ni Mkadarasi wa Ujenzi Injinia Thedeus
Koyanga (mwenye shati la mikono mirefu) akifuatiwa na Profesa Ernest
Kihanga Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Utawala na Fedha.
Mhe. Waziri Ndalichako akiongozwa
na Mkandarasi wa mradi akikagua vyuma vya madarasa mara alipowasili
kukagua ujenzi wa jengo la ghorofa tano la Taaluma na Utawala
linalotazamiwa kumalizika mwezi Juni,2019. Pamoja naye ni Makamu Mkuu wa
Chuo Kikuu Mzumbe Prof. Lughano Kusiluka, Naibu Mawakamu Mkuu wa Chuo
Utawala na fedha Prof. Ernest Kihanga na wasimamizi wa ujenzi.
Mhe. Profesa Joyce Ndalichako
alikagua muonekano wa nje wa jengo la Taaluma na Utawala la chuo Kikuu
Mzumbe Kampasi ya Mbeya pamoja na kukagua usafi wa mazingira, alipofanya
ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi kabla Mhe. Rais Dkt John Pombe
Magufuli hajafika kuweka jiwe la msingi.
……………………..
Waziri wa Elimu, Sayansi,
Teknolojia na Ufundi Mhe. Prof. Joyce Ndalichako leo ametembelea na
kukagua hatua za maandalizi ya ujenzi wa Jengo la Taaluma na Utawala la
Chuo Kikuu Mzumbe Kampasi ya Mbeya, ambapo amepongeza Uongozi wa Chuo
Kikuu Mzumbe kwa hatua za ujenzi ulipofikia.
Akiwa ameambatana na Kaimu Mkuu wa
Chuo hicho Pro. Lughano Kusiluka, Prof Ndalichako amemwelekeza
Mkandarasi wa Ujenzi kuhakikisha kufikia Juni 2019 ujenzi wa Jengo hilo
kuwa umekamilika kama ilivyopangwa.
Kukamilika kwa ujenzi kutawezesha
jumla ya wanafunzi 900 kupata vyumba vya madarasa mbali na kumbi za
mikutano na ofisi za uendeshaji. Jengo hilo linatarajiwa kuwekwa jiwe
la Msingi na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John
Joseph Magufuli Mei 1, 2019.
No comments :
Post a Comment