Mwenendo bora wa madaraka ya
serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania chini ya Rais Dk. John Pombe
Magufuli umepelekea kampuni ya State Oil kuweka bayana mafanikio na
utofauti wa awamu ya tano.
Hayo yamebainishwa na mkurugenzi
mtendaji wa State Oil Tanzania Limited Anil Suchak katika mahojiano na
mwandishi wa gaazeti la Jamhuri Jijini Dar es salaam ambapo
alisema
kwamba serikali ya awamu hii imefanya mabadiliko makubwa katika kipindi
kifupi tofauti na matarajio yaa wengi pia kwenye biashara kuna maboresho
makubwa katika bandari ya Dar es salaam.
Hata hivyo State Oil ni Kampuni
maridhawa nchini na ni kongwe katika masuala ya mafuta, kwenye mahojiano
hayo Mkurugenzi Suchak aliweka bayana mwenendo wa biashara hiyo ndani
ya serikali ya awamu ya tano
“Ukweli ni lazima usemwe, hakuna
kipindi kizuri cha biashara kama hiki, hapo awali tulikuwa tukikumbana
na vikwazo lakini sasa hatuna tatizo ukizingatia kumekuwepo na ongezeko
la uingizaji mafuta ndani ya miaka mitatu(2015-2018) kwa asilimia 11,
kwa mwaka jana 2018 usafirishaji wa mafuta nje ya nchi ulikuwa asilimia
14, wakati mwaka 2015 ulikuwa ni asilimia 2 pekee, tunaamini mpaka
kufikia mwaka 2020 kiwango kitaongezeka zaidi”Alisema Mkurugenzi Suchak
Aidha Suchak aligusia mageuzi
mengine yaliyofanywa na serikali ya awamu ya tano na kutoa pongezi
ambapo ni ujenzi wa ukuta, machimbo ya madini ya Tanzanite, Mradi wa
kihistoria wa kufua umeme Stiegler’s Gorge, kufufuliwa kwa shirika la
ndege (ATCL), Mradi mkubwa wa reli(SGR) na maboresho ya vituo vya Afya.
“Ninampongeza sana Mhe.Dk.
Magufuli kwa jitihada zake na kuamua kwa dhati kutekeleza miradi hii
mikubwa, kutokana na kasi hiyo nchi yetu sasa inaenda kwenye uchumi wa
viwanda, na licha ya nchi yetu kuwa na vyama vingi ni jukumu la kila
mtanzania kuungana ili kuisaidia serikali lango la kujenga nchi”
Ikumbukwe kuwa Tanzania ni
miongoni mwa nchi zilizobarikiwa kuwa na rasilimali za kipekee duniani
licha la rasilimali hizo nchi imekuwa tegemezi,. Mwaka 2015 Tanzania
ilifanya uchaguzi na Dokta John Pombe Magufuli akachakuliwa kuwa rais wa
awamu ya tano ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania na serikali imekuwa
ikitekeleza miradi mikubwa ya maendeleo ambayo waau mbalimbali
wameipongeza kwa mafanikio.
No comments :
Post a Comment