Wednesday, April 24, 2019

DREAMLINNER YA MAGUFULI KUANZA SAFARI ZA MUMBAI INDIA MWEZI JULAI


1
Mkuu wa Mawasiliano wa Shirika la ndege la (ATCL) Bw Josephat Kigirwa.
……………………………………………………………………………
Ndege ya Shirika la Ndege la Air Tanzania (ATCL) Boeing 787-8 Dreamlinner  inatarajia kuanza  safari zake za nje ifikapo  Julai mwaka huu, Akizungumza na waandishi wa habari Mkuu wa Mawasiliano wa Shirika hilo Bw. Josephat Kigirwa amesema safari hizo zitaaza tarehe 17  mwaka huu ambapo sambamba na safari  za india  pia Juni 28 wataanza kutoa huduma kati ya  usafiri wa Johnsburg Afika Kusini na Dar es salaam safari zikiwa mara tatu kwa wiki.
Ameongeza kuwa huo ni mwendelezo wa mpango wao mahsusi wa kupanua huduma za shirika hilo humu nchini na nje ya nchi ambapo kwa sasa tayari wanatoa huduma katika mikoa 10 ya Tanzania  ikiwemo Kilimanjaro, Mbeya, Kagera, Kigoma, Mbeya, Mwanza, Dodoma,Tabora, Shinyanga na Zanzibar, Kwa sasa tayari  (ATCL) inatoa  huduma ya usafiri wa anga katika nchi 4 mpaka sasa ambazo ni Bujumbura Burundi, Entebe Uganda, Lusaka Zambia na Harare Zimbabwe.
Josepaht Kigirwa ameongeza kuwa kwa sasa wanafanya tafiti mbalimbali na matayarisho  ili kuanzisha safari zingine nchini ambapo wiki ijayo wataanza safari katika mkoa wa Iringa na tayari wako katika utaratibu wa kujiweka sawa kwa ajili ya kuongeza huduma katika Viwanja vya Mpanda Katavi, Mtwara mkoani Mtwara, Songea Mkoani Ruvuma, Pemba Zanzibar na mkoa waTanga.
2
Waandishi wa habari wakimsikiliza Mkuu wa Mawasiliano wa Shirika la ndege la (ATCL) Bw Josephat Kigirwa.
3
Mkuu wa Mawasiliano wa Shirika la ndege la (ATCL) Bw Josephat Kigirwa akisisitiza jambo wakati alipozungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kuhusu kuanzishwa kwa safari za India na Afrika ya Kusini.

No comments :

Post a Comment