Wednesday, April 24, 2019

CCM MKOA WA MAGHARIB YATUA JIMBO LA KIEMBESAMAKI

IMG_3485
KAMATI ya Siasa ya CCM Mkoa wa Magharib wakikagua mradi wa Maji Safi na Salama uliotekelezwa chini Mfuko wa Jimbo la Kiembe Samaki katika ziara yao ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM.
IMG_3489
DIWANI wa Wadi ya Mbweni Unguja Ndugu Maabadi Ali Maulid akitoa maelezo juu ya usambazaji wa mipira ya maji Safi na Salama katika maeneo mbali mbali ya Wadi hiyo.
………………………………………………………………………………………
NA IS-HAKA OMAR,ZANZIBAR.
CHAMA Cha Mapinduzi(CCM) Mkoa wa Magharibi Unguja kimewataka viongozi wa Jimbo la Kiembe Samaki kuongeza kasi ya utekelezaji wa Ilani ya CCM ili kutatua changamoto zinazowakabili Wananchi.
Rai hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa huo Ndugu Mohamed Rajab Soud katika mwendelezo wa ziara ya Kamati ya Siasa ya Mkoa ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM katika Jimbo la Kiembe Samaki.
Alisema pamoja na kutekelezwa kwa miradi mbali mbali ya maendeleo kupitia fedha za mifuko ya maendeleo ya Jimbo hilo bado kupanahitajika juhudi za ziara za kutatua kero za wananchi katika sekta za Afya,Maji Safi na Salama pamoja na miondombinu ya barabara za ndani.
Alisema lengo la ziara hiyo ni kukagua miradi inayotekelezwa na viongozi hao kama thamani ya fedha zinazoandikwa katika ripoti ya maendeleo ya Jimbo zinaendana na fedha iliyotumika.
Aliwambia viongozi hao kuwa wahakikishe miradi wanayoitekeleza isaidie jamii husika badala ya watu wachache.
Aidha amewasihi Wananchi wa Jimbo hilo kuithamini na kuitunza miradi mbali inayotekelezwa kupitia Ilani ya CCM ili iwanufaishe vizazi vya sasa na vijavyo.
“Utekelezaji wa Ilani ya CCM ndani ya Jimbo la Kiembe Samaki unafanuyika lakini bado sijaridhika kwa baadhi ya maeneo hivyo wahusika wanatakiwa kuongeza kasi kubwa katika kutatua kero za wananchi.”,alieleza Mwenyekiti huyo Mohamed.
Naye Diwani wa Wadi ya Mbweni Ndugu Maabadi Ali Maulid amesema katika kutatua kero za wananchi wamejipanga kutekeleza miradi mikubwa mitatu ikiwemo kutengeneza minara mitatu katika visima vya maji ili wananchi wapate huduma hiyo kwa wakati.
Naye Afisa Mipango Manispaa ya Magharib ‘B’ Ndugu Saumu Daniel Yussuf akizungumza katika Kituo cha Afya cha Kiembe Samaki alisema wanaendelea kuimarisha huduma za Afya katika Vituo mbali mbali licha ya kukabiliwa na changamoto za uchakavu wa majengo waliokabidhiwa katika mfumo wa ugatuzi.

No comments :

Post a Comment